WIZARA YA AFYA YATOA UFAFANUZI KUHUSU DAWA BANDIA YA UKIMWI
Ili kuondoa mkanganyiko ambao umeanza kujitokeza, Wizara inapenda kutoa
ufafanuzi kuhusu tamko lililotolewa na Mhe. Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii. Aidha, kama ilivyoelezwa katika taarifa mbalimbali za umma
zilizokwisha kutolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na
TFDA kuhusiana na suala hili, bado inasisitizwa kwamba kampuni ya TPI Ltd
iliiuzia Bohari ya Dawa (MSD) dawa bandia aina ya TT-VIR 30 toleo Na.
0C.01.85, kwa mujibu wa nyaraka zilizopo.Tunapenda kusisitiza kwamba,
Mhe. Waziri katika hotuba yake hakukanusha kuwa kampuni ya TPI Ltd iliiuzia
MSD dawa hizo bandia. Aidha alieleza kua vyombo vya habari bado vinaendelea na utafiti ili kujua chanzo cha na wahusika wakuu wa dawa hizo bandia.Kuzingatia hasa na unyeti wa suala lenyewe wizara inaasa vyombo vya habari kuwa na subira ili kuepuka kutoa taarifa ambazo zitapotosha jamii.Hii ni kauli ya msemaji mkuu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii.
No comments:
Post a Comment