Jumamosi ya June 8 ilikuwa ni ya kihistoria kwa muziki wa Tanzania
kwakuwa pamoja na kutolewa tuzo za KTMA, wasanii wawili, Noorah na
H.Baba walifungua ndoa na kuisaliti rasmi kambi maarufu mjini ya
makapela.
Noorah akiwa na mke wake
Harusi ya Noorah ilifanyika mkoani kwao Shinyanga na ameiambia Bongo5 kuwa ilienda vizuri na kila mmoja alifurahi.
“Kwangu mimi kiukweli ni ya kihistoria sana kwasababu kila mtu
alikuwa happy. Unajua shughuli kama hii ni ya watu wengu, shughuli ikiwa
na watu wengi halafu watu wote wakafurahi inakupa faraja kubwa sana
hata wewe mwenyewe,” amesema Noorah ambaye mke wake anaitwa Camilla.
Noorah akiwa amembeba mke wake
“Ndoa ni commitment, ndoa ni majukumu, ndo ni vitu kama hivyo sasa
kama nimefika hatua ya kuweza kudiriki kuthubutu kitu kama hicho maana
yake najiona kwamba nimekomaa vizuri.”
Kwa upande wake H.Baba aliyefunga ndoa na mpenzi wake siku nyingi,
Flora Mvungi ambaye ni muigizaji wa filamu, ameiambia bongo5 kuwa tangu
aingie kwenye maisha ya ndoa Jumamosi iliyopita amekuwa ni mtu mwenye
furaha na amani wakati wote.
H.Baba akiwa na mke wake Flora Mvungi na Wastara
“Maisha ya ndoa ni mazuri sana, kumbe nilikuwa sifahamu waliopo
kwenye ndoa wana furaha kubwa sana,maisha ya ndoa yana faraja, yana
amani, yaani tangu nilipochukua jiko langu Jumamosi nina furaha
sana,”alisema H.Baba ambaye jina lake halisi ni Hamis.
H.Baba akisaini cheti cha ndoa
Pia amewaambia vijana na wasanii wenzake waache woga kwani ndoa
haitaji gharama kubwa na kwamba kila mmoja akiamua anaweza akafanya.
“Mimi nawakaribisha wasanii wenzangu na vijana katika maisha ya ndoa
kwasababu mimi nyenyewe nimekaribishwa, pia kuna watu walio
nitangulia, kaka zetu ,dada zetu, kwahiyo mimi nawaombea na waungane na
sisi. Kwasababu hili ni jambo la heri ni jambo ambalo limepangwa katika
maisha kwamba kijana akifikia umri wa kuoa basi lazima uoe, unajua usioe
wakati upo mzee, usioe wakati umefulia unajua kuna watu wanasubiri
washuke ndipo wanaoa hawajui msanii ni kioo cha jamii, siyo unakaa na
kuchafua dada za watu bila sababu, sisi ni wasanii tunaangaliwa na watu
wengi kwahiyo tujifunze.”
Kuanzia Kushoto: Pasha, H.Baba, Flora na Wastara
No comments:
Post a Comment