Kuna mambo mawili yanaleta tafakari isiyo na ulinganifu japokuwa yaweza kuwa na mwelekeo unaofanana, ila kiuhalisia unakinzana.
Mosi, baada ya kutangazwa rasmi kuwa Tanzania itapeleka majeshi yake
Congo, waasi wa M23 wameitaka Tanzania isipeleke jeshi lake huko.
Kwanini M23 wanapinga sana Tanzania kuleka jeshi lake huko? Kwanini
kelele zao ni kubwa sana kwa Tanzania lakini wako kimya kwa mataifa
mengine? Je! Ni kwamba wanaiogopa Tanzania ama wanaionea huruma
Tanzania, kuna nini kati ya nchi hizi mbili?
Pili, pamoja na kukatazwa kwenda Congo na M23, kwanini Tanzania
tunang'ang'ania kupeleka jeshi huko? Pamoja na hali ngumu ya kiuchumi
tuliyonayo watanzania kwanini Nshodha na Membe wanasisitiza jeshi letu
kwenda huko? Ok, mtu aweza kusema kwasababu Rais alikubali kupeleka
jeshi. Je kwanini Rais akubali kirahisi kupeleka jeshi Congo wakati
suala kulitoa jeshi nje ya mipaka yako ni suala lenye kuhitaji tafakari
kubwa zaidi.
No comments:
Post a Comment