Spika wa Bunge Mh.Anna Makinda amelazimika kusitisha shughuli za bunge mwanzoni tu mwa
hotuba ya kambi rasmi ya upinzani iliyokuwa ikisomwa na waziri kivuli
wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Joseph Mbilinyi aka
Sugu.
Kauli kwenye hotuba hiyo iliyobabisha spika wa bunge asitishe shughuli
za leo hadi jioni ilisema, “Tanzania imegeuka chini ya usimamizi wa
wizara ya serikali hii ya CCM kuwa taifa linalotoka nyara wanahabari,
kuwatesa, kuwangoa kucha na meno, kuwatoboa macho, kuwamwagia tindikali
na hata kuwaua.”
Spika amesitisha bunge hilo ili kupata muda wa kuipitia hotuba hiyo kuondoa kauli za uchochezi.
No comments:
Post a Comment