Friday, 24 May 2013

WAASI WA M23 WATISHIA KUTUVAMIA MUDA WOWOTE.


WAASI WA M23 WATISHIA KUTUVAMIA MUDA WOWOTE....SERIKALI YA MKOA WA KAGERA YATOA TAHADHARI KWA WANANCHI


Serikali ya Mkoa wa Kagera imewatahadharisha wananchi wake kuepukana na wageni wasiowafahamu kwenye maeneo yao kutokana na tishio la kikosi cha M23 cha nchini Congo DRC kinachotishia kuivamia Tanzania...
Kumekuwa na mapigano makali kati ya waasi wa M23 na vikosi vya serikali nchini Congo ambako jeshi letu lipo huko...
Waasi hao wametishia kuivamia Tanzania muda wowote ili kulipiza kisasi.Miongoni mwa mipaka ambayo iko wazi ni Kagera, na hii ndo sababu iliyopelekea serikali ya Mkoa huo kutoa tahadhari kwa wananchi wake na watanzania kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment