Friday, 31 May 2013

NEWZ:AJALI YATOKEA BAADA YA KUJARIBU KUDANDIA DALADALA

Afariki baada ya kuanguka akidandia daladala, Dar

afariki-akidandia-daladala-0
afariki-akidandia-daladala
Mtu mmoja ambaye jina lake bado halijafahamika, amefariki dunia baada ya kuteleza na kuanguka wakati alipokua akijaribu kudandia Daladala maeneo ya Ilala Boma, Jijini Dar es Salaam, asubuhi leo. Marehemu huyo baada ya kuanguka na kupiga kichwa kwenye lami, alipasuka kichwa na kuvuja damu nyingi kichwani, na kufariki katika eneo la tukio.

Mwili wa marehemu umepelekwa katika Hospitali ya Amana, Ilala.
 Wasamaria wema wakisaidia kumpakia kwenye gari kwa kumpeleka hospitalini
                
Damu ya marehemu ambayo kwa kiasi kikubwa imetoka kichwani baada  ya kupasuka vibaya
Mwili wa marehemu ukiwa tayari kuondolewa kwenda hospitali
               
Hii ndio daladala ambayo marehemu alikuwa akitaka kudandia na kudondoka kwa bahati mbaya
Umati wa watu ukishuhudia ajali maeneo ya Ilala Boma asubuhi hii
                                   

No comments:

Post a Comment