Tuesday, 14 May 2013

WILLIAM RUTTO NA MKEWE WAWASILI HAGUE UHOLANZI

WILLIAM RUTTO NA MKEWE WAWASILI HAGUE UHOLANZI

Naibu wa rais William rutto na mkewe Recho rutto wamewasili katika mahakama ya mataifa Hague uholanzi tayari kwa kikao cha leo na wahusika kwenye kesi ya jinai inayo mkabili bwana Rutto.
kwenye kikao cha leo, maswala kama ombi la Rutto kutaka kesi yake kuahirishwa hadi Novemba mwaka huu kutoa nafasi kwa mawakili wake kujiandaa zaidi. Rutto pia anaomba kuhudhuria vikao vya kwanza na mwisho na kutaka mtandao na video link kutumika kwenye vikao vinginevyo kumwezesha kujukumika na maswala ya kuongoza taifa.
upande wamastaka pia umetoa ombi kwa majaji, kuwaongeza mashahidi wengine watano kutilia makali kesi hiyo.
Rutto na mwanahabari Joshua sang wanatuhumiwa kupanga kufadhili na kuelekeza mashambulizi dhidi ya wafuasi wa chama cha PNU punde baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007 uliokumbwa na utata baada ya Rais mstaafu Mwai kibaki kutangazwa.
Rais Uhuru kenyatta kwa upande wake anatuhumiwa kwa kosa la kufadhili mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya wafuasi wa ODM Naivasha na Nakuru mkoani Rift valley.
by Story In Courtesy Of julius kipkoech from Nairobi Kenya

No comments:

Post a Comment