Thursday, 16 May 2013

MWIGIZAJI ANGELINA JOLIE AONDOLEWA KIZAZI


Baada ya kufanya upasuaji wa kuondoa matiti yake yote mawili, Angelina Jolie anapanga kufanya upasuaji wa kuondoa kizazi kwakuwa ana asilimia 50 ya hatari ya kupata kansa iliyochukua maisha ya mama yake.
Muigizaji huyo mwenye miaka 37 alichukua uamuazi huo wa kishujaa uliohusisha mchakato wa miezi mitatu baada kubaini kuwa ana asilimia 87 ya kupata kansa matiti. Na sasa Angelina anasemekana kuwa ameshapanga kufanyiwa upasuaji mwingine kwa kuondolewa ovary zake zote mbili kwakuwa ana uwezekano mkubwa wa kupata kansa ya kizazi.

Kwa mujibu wa jarida la People, Angelina anaweza kufanya upasuaji huo kabla hajatimiza miaka 40. Baada ya upasuaji huo, Angelina hatoweza tena kuzaa.

Yeye na mchumba wake Brad Pitt wana watoto watatu wa kuzaa Shiloh na mapachsa Knox na Vivienne, pamoja na watatu wa kuasili Maddox, Pax na Zahara.

No comments:

Post a Comment