HIZI NDO HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE..
Albert Mangwea 'Ngwair' na M to the P |
Kwa kuwa ripoti zinapatikana kutoka Afrika kusini na
wachache sana ndio wenye mawasiliano ya moja kwa moja na watu walioko
hospitalini hapo na hadi sasa hakuna mzungumzaji maalum aliyeteuliwa kutoa
taarifa kutoka hospitalini hapo, inaweza kuwa chanzo cha habari kutofautiana.
Kwa waliosikiliza TBC Taifa saa kumi katika kipindi cha
‘harakati’ wametangaza kuwa M to the P amefariki dunia asubuhi ya leo na
mipango ya kusafirisha miili ya wawili hao inaendelea.
Lakini habari za uhakika zilizopatikana ni kwamba msanii
huyo bado yuko hai japokuwa hali yake ni mbaya sana.
Msanii Bushoke na baadhi ya ndugu wa marehemu tayari wako
Afrika kusini na ripoti zilizopatikana kutoka kwao zinasema msanii M to the P
anaendelea vizuri, japo alikuwa anapumulia mashine alipowaona alipata nguvu
akanyanyuka kidogo akiwa pale pale kitandani.
Millard Ayo mtangazaji wa kipindi cha amplifaya cha Clouds
Fm ambae yuko katika hospitali ya St. Hellen Johannesburg, amethibisha kuwa M
to the P yuko hai. Hii ni tweet yake muda mfupi uliopita.
“#BREAKING Sio kweli kwamba m2theP kafariki, ni mzima ila
anapumulia mashine, kafungua macho na kunyanyua miguu dakika chache
zilizopita.”
Watanzania waliofika hospitalini hapo wamepata nafasi ya
kuuangalia mwili wa marehemu na wanasema walikuwa nae hadi jana majira ya saa
kumi jioni, inasikitisha sana.
Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu bado inaendelea.
No comments:
Post a Comment