KAULI YA ZITTO KABWE KUHUSU WIZARA YA MADINI NA NISHATI
Kesho
jumamosi wabunge tumealikwa kwenye semina kuhusu sera ya Gesi Asilia.
Tumegawiwa tayari nakala zetu, tena zipo kwenye lugha ya kimombo.
Ikumbukwe kwamba kuanzia tarehe 22 - 23 Mei 2013 kutakuwa na mjadala wa
bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini. Semina hii Ni maandalizi ya
Bajeti hii.
Jambo la kushangaza Ni kwamba wakati sera ya Gesi Asilia ipo
kwenye rasimu na ndio kwanza wabunge tumeletewa kutoa maoni, Serikali
tayari imetangaza tena kugawa vitalu vya Mafuta na Gesi kwenye Bahari
kuu na Ziwa Tanganyika Kaskazini. Zabuni hii mpya ya vitalu vya
utafutaji imetolewa wakati kuna maamuzi ya Bunge kuzuia ugawaji huu mpya
mpaka sera ya Gesi Asilia na Sheria ya Gesi vikamilike. Haraka hii ya
serikali kugawa vitalu bila sera wala Sheria inatoka wapi?
Nitashangaa
sana wabunge kukimbilia posho za semina hii na kuhalalisha maamuzi
yasiyo zingatia maslahi ya Taifa Kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Uamuzi
wa kugawa vitalu vipya bila kwanza kuwepo Kwa sera na Sheria mpya
unapaswa kupingwa Kwa Nguvu zote. Tafuta mbunge wako, mwambie asikubali
maamuzi haya ya serikali. Tumalize kwanza sera na Sheria ndio tugawe
vitalu vipya. Gesi sio viazi, haiozi.
No comments:
Post a Comment