Linah na Barnaba kuna uwezekano wakatimuliwa THT... SHUKA NAYO HAPA.
KUELEKEA
shoo maalumu ya Miaka 13, ya mwanamuziki nguli wa bongo fleva nchini na
kiongozi wa bendi yenye msisimko mkubwa ya ‘Machozi Band’, Judith
Wambura ‘Lady Jay Dee’ au Jide’ huenda kwa upande wa wasanii wa Nyumba
ya Vipaji ya THT, Linah Sanga na Barnaba mwaka huu ukawa mchungu kwao
kufuatia kuwepo taarifa za kutimuliwa na uongozi wa juu.
Kwa
mujibu wa vyanzo kutoka kwa mtu wa karibu wa Linah kilieleza kuwa mpaka
sasa msanii huyo hana raha na wala hajui ataanza vipi katika harakati
zake za kimuziki hasa kufuatia hivi karibuni kukacha shoo ya nguli Lady
Jay Dee kwa shinikizo kutoka kwa wakubwa zake.
Hata
hivyo, Linah inadaiwa uongozi wa juu umekaa kikao na hatua iliyofuatia
kwenye kikao hicho ni kuwaondoa kabisa kwani huenda wakatia doa wasanii
wenzao ndani ya kundi hilo.
“Juzi
Lina,haikuwa kawaida yake maana hata alipopigiwa simu na kwa ajili ya
hatua zingine alionekana kuw na hofu, na wala hakutaka kusikia ushahuri
wangu ambao nilikuwa nikimhusia kuwa aachane na mawazo hayo kwani jambo
analoliwaza huenda likaisha na hata maamuzi yatakayotoka yatakuwa ni
kawaida” kilieleza chanzo kutoka kwa mtu wakaribu wa Lina, amabaye hata
hivyo alisema kuwa huenda ukweli wa jambo ukawa hadharani.
Hata
hivyo taarifa za ndani za uongozi wa THT zilibainisha kuwa mpango wao wa
kuwashughulikia wasanii hao upo pale pale na taratibu zinafuata
ilizisilete madhara kwa wasanii waliopo ndani ya THT na watu wa karibu
wanaoiunga THT.
“Wewe
nani kakwambia kama tumewaadhibu Lina na Barnaba?, ndio kwanza
tunakusikia wewe hizo taarifa, sisi tunafanya mambo yetu wao waache
wafanye yao tukiwa nao sie na tunaouwezo wa kuwatimua ilikulinda hadhi
ya THT” Kilieleza chanzo hicho ambacho hata hivyo kutokana na usalama wa
jina lake tumelihifadhi. Ambapo namba yake inaishia na**08.
Aidha,
katika ‘ku-balance’ huondo kamili wa habari hizi wasanii hao wote
walipotafutwa kwenye simu zao za mkononi lakini hawakuweza kuwa hewani
kwa muda mrefu.. na hata alipopigiwa mtu wao huyo wa karibu naye alizima
simu.
Katika
kile kinachoeleza kupamba moto shoo hiyo, na kujaa kwa taarifa
mbalimbali juu ya wasanii watakaopamba shoo ya miaka 13, Mei 31 ndani ya
Nyumbani Lounge, Tayari tiketi zimeanza kuuzwa maeneo mbalimbali ya
jiji la Dar es Saalam.
Shoo
hiyo ya kijanja Nyumbani Lounge, patakuwa hapatoshi pale wadau wa
burudani na wastaarabu wote watakapojumuika kwa pamoja ku-shoo love kwa
Lady Jay Dee na Machozi Band, huku listi ya mastaa mbalimbali
wanatarajia kuudhuria sambamba na ‘surprise’ kutoka kwa mastaa hao ambao
kwa sasa wengi wapo kimya wakihofia kutengwa na wazee wa ‘fitina bin
Logiki’.
Awali
kulikuwapo na taarifa za kuwapo kwa msanii Matonya, ambaye hata hivyo
mtandao wa Lady Jay Dee ulitoa hadharani kuwa mwanamuziki huyo
ameshachukua ‘advance’ ya shoo hiyo na wazee wa ‘kuingilia logik’
wameshamtisha Matonya ili ajitoe, lakini akiwa ameshatafuna pesa ya
watu.
Mtandao
huo wa kijamii blog, ilinukuu kila kitu juu ya Makubaliano baina ya
Capt.Gadna G Habashi na Matonya ambapo pia unaweza kuyasoma kupitia
(Ladyjaydee.blogspot.com) Pia ulitoa kwa mara ya kwanza picha,maelezo
muhimu na video ya wanamuziki hao wawili Linah na Barnaba wakiingia
mkataba wa shoo hiyo na pia kuhamasisha watu kufika Mei 13.
No comments:
Post a Comment