TAARIFA YA KIFAMILIA KUHUSU MAZISHI YA NGWEA NA JINSI MWILI HUO UTAKAVYOLETWA TANZANIA
Baba
Mdogo wa Marehemu Mzee Mangweha ambaye yuko Mbinga Songea kikazi,
amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake mkubwa yaani baba mkubwa wa
Ngwair, David Mangweha ambaye naye yuko Songea kuwa watu watakutanika
Mbezi kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika hapa Dar es salaam Mbezi
Beach.
Ingawa
bado kikao cha familia nzima hakijafanyika lakini baba huyo mdogo
amesema wanaweza kulazimika kuzika Morogoro sehemu ambayo baba yake
alizikwa.
Baba huyo mdogo alisema kuwa kesho ndo watarudi Dar es Salaam pamoja na kaka yake yaani baba mkubwa wa marehemu.
Kuhusu
mwili kuletwa hapa Tanzania kutoka Afrika Kusini baba mdogo amesema
kuwa mpaka sasa hawajajua jinsi gani mwili huo utafika hapa lakini kuna
ndugu zao ambao tayari washaanza kufanya taratibu za kuwasiliana na
ubalozi wa Afrika Kusini ili kujua ni jinsi gani mwili huo utafika hapa.
Kama kutakuwa na mabadiliko yeyote watakapowasili kesho baba mdogo na baba mkubwa baada ya kikao cha familia watatoa taarifa.
No comments:
Post a Comment