Shuka nayo apa.....
RISASI LATUA KIJITONYAMA
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilisaga soli hadi maeneo
hayo na kuanza kugonga geti moja baada ya lingine hadi lilipofanikiwa
kuinasa nyumba hiyo huku Nisha akiwa ndani kapumzika.
Msichana
aliyejitambulisha kuwa ni dada wa kazi au hausigeli kwa lugha laini
ndiye aliyetoboa siri kuwa ni kweli staa huyo yupo ndani na amehamia
mahali hapo muda si mrefu.
Ndani
ya nyumba hiyo yenye vyumba vitano, sebule, jiko, choo na mabafu mawili,
anayeishi Nisha na dada wake wa kazi, kuna samani nyingi za bei mbaya,
mazagazaga kibao, mazulia na marumaru huku kila kona kukiwa na Tv ya
flat screen hadi chooni (angalia picha Uk.1).
Nisha anayemiliki kampuni ya kuzalisha muvi za Kibongo ya Nisha’s Film
Production alipotakiwa kueleza kama kanunua, kanunuliwa au kapangisha
nyumba hiyo, alikuwa na haya ya kusema:
“Ni juhudi zangu binafsi
jamani, kujituma sana kwenye kazi yangu ya filamu. Kuhusu kununua au
kupangisha naomba nikimaliza ‘process’ f’lanif’lani ndipo nitaweka wazi,
kwa sasa bado ni mapema mno.”
No comments:
Post a Comment