MICHEZO

 24, 2013

AMRI KIEMBA NA SURE BOY NDIO WANASOKA BORA WA TANZANIA


 Katibu Mkuu wa Chama cha Wachezaji Mpira Tanzania (SPUTANZA), Said George, akiongea huku akiwa na baadhi ya viongozi wenzake wa chama hicho wakati wa utoaji wa tuzo za wachezaji Bora wa Chama hicho kwa mwaka 2013, ukumbi wa Diamond Jubilee usiku wa kuamkia leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-bayana.blogspot.com)
Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani, akizungumza wakati alipokuwa akifungua utoaji wa tuzo ya Mwanasoka bora wa SPUTANZA, ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Said George.
Baadhi ya vingozi wa Kishen Enterprises, moja ya wadhamini wa tuzo hizo, wakiwa katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo, ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
 Wasanii wa Sky Light Band wakitumbuiza katika utoaji wa tuzo hizo, ukumbini humo.
Mkurugenzi wa Kishen Eterprises, wauzaji wa pikipiki za Lifan, ambao ni moja ya wadhamini wa tuzo hizo, Rajen Solank (kushoto), akimkabidhi Meck Mexime tuzo ya kocha bora wa msimu.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah, akiongea kabla ya kumtaja mchezaji boara anayechipukia, ambaye alikuwa Salum Abubakar tuzo ya Sputanza, baada ya kuwashinda wenzake kadhaa katika katagoria hiyo.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah, akimkabidhi mchezaji boara anayechipukia, Salum Abubakar tuzo ya Sputanza, baada ya kuwashinda wenzake kadhaa katika katagoria hiyo.
Mwenyekiti wa SPUTANZA, Mussa Kissoky, akimkabidhi tuzo ya golika bora Kocha wa Mtwibwa, Mecky Mexime.
Mkurugenzi wa Kishen Eterprises, wauzaji wa pikipiki za Lifan, ambao ni moja ya wadhamini wa tuzo hizo, Rajen Solank (kulia), akizungumza kwa ajili ya kumtambulisha kwa mashabiki wa Mwakilishi wa Kampuni ya Lifan, Nasikiwa Benya (kushoto), wakati wa hafla hiyo. Katikati ni Katibu Mkuu wa SPUTANZA, Said George.
Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani, akipanda kuijaribu pikipiki ya kike, aliyozawadiwa mke wa Rais, Mama Salma Kikwete na kukabidhiwa yeye na Mkurugenzi Kishen Enterprises, katika hafla hiyo usikuwa wa kuamkia leo, ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani, akikabidhiwa zawadi na Mmoja wa wanafamilia ya Pepsi, ambao ni moja ya wafadhili wa tuzo hizo, Fadi El-Khalil.
Wanafamilia ya Pepsi, Fadi El-Khalil (kulia) na Meneja Mkuu wa Uhasibu Taifa wa Kampuni ya Pepsi, ambao ni moja ya wafadhili wa tuzo hizo, Bhank Patwa, wakifungua bahasha yenye jina la mchezaji bora wa jumla SPUTANA, ambapo Amri Kiemba wa Simba aliibuka kinara.
Meneja Mkuu wa Uhasibu Taifa wa Kampuni ya Pepsi, ambao ni moja ya wafadhili wa tuzo hizo, Bhank Patwa (kushoto), akiwa na mwanafamilia ya Pepsi, Fadi El-Khalil (katikati), akimkabidhi Mohamed Bhinda kwa niaba ya mchezaji bora wa jumla wa SPUTANA, Amri Kiemba wa Simba ambaye hakuwepo katika hafla hiyo.

HISPANIA YAPIGA MTU 10-0, TORRES APIGA 4

Wakati mashabiki wengi wakidhani Mabingwa wa soka duniani, timu ya taifa ya Kispania wangewafunga Tahiti mabao zaidi ya 10, hatimaye watoto wa Tahiti wamekaza na kuwazuia vilivyo wapinzania wao na kufungwa maboa 10-0 tu.
Mshambuliaji  Fernando Torres amefunga mabao manne pamoja na kukosa penalti wakati Hispania ikiifumua 10-0 Tahiti katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mabara.
Alifunga mabao hayo katika dakika za tano, 33, 57 na 78 wakati David Villa alipiga Hat-trick katika dakika za 39,49 na 64, David Silva akafunga mawili dakika za 31 na 89 na Juan Mata pia akafunga dakika ya 66 kuiwezesha Hispania kupaa kileleni mwa Kundi B mbele ya Nigeria, ambao muda huu wanamenyana na Uruguay.
Kikosi cha Hispania kilikuwa: Reina, Albiol, Azpilicueta, Ramos/Navas dk46, Monreal, Martinez, Cazorla/Iniesta dk76, Silva, Villa, Torres na Mata/Fabregas dk69.
Tahiti: Roche, Ludivion, Vallar, Lemaire/Vero dk73, Aitamai, J Tehau, A Tehau/T Tehau dk53, Vahirua, Caroine, Bourebare/L Tehau dk69 na Chong Hue.
Here we go: Fernando Torres was on fire for Spain against Tahiti as the world champions eased to a winMoto wa nguvu: Fernando Torres alikuwa hatari katika mchezo wa usiku wa kuamkia leo dhidi ya Tahiti
Me too: Barcelona striker David Villa also showed no mercy to the part-timers Hata mie: Mshambuliaji Barcelona  David Villa  naye alionesha kiwango cha juu
Caught out: Torres slid the ball in at the near post to put Spain in the lead early in the match Kazi yaanza: Torres akitumbukiza goli la kwanza
CONFEDERATIONS CUP GROUP B

Team Played Won Drawn Lost For Against Points
Spain 2 2 0 0 12 1 6
Nigeria 2 1 0 1 7 3 3
Uruguay 2 1 0 1 3 3 3
Tahiti 2 0 0 2 1 16 0
And another one: Torres rolled home his second of the night and Spain's third Lingine tena: Torres akiandika kimiani bao la pili
Understated: Torres and his team-mates look underwhelmed after the Chelsea striker netted their sixth



 KAMA ULIKUA HAUJUI HII HAYA NDIO MAPATO YALIYO PATIKANA KATIKA MICHI KATI YA TAIFA STARS NA IVORY COAST

Mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Ivory Coast uliingiza sh. 502,131,000 kutokana na watazamaji 57,203 walioshuhudia mpambano huo. Kwa mujibu wa taarifa ya TFF mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa:
18% ya VAT ni sh. 76,596,254.24 ,
Gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,809,104,
15% ya uwanja sh. 62,658,846.26,
20% ya gharama za mechi sh. 83,545,128.35 na asilimia
5% ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 20,886,282.09.
60% ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 250,635,385.06 na
5% Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,531,769.25

 

Uzoefu mdogo wa Stars yaipaisha Ivory Coast

Mshambuliaji wa Taifa Stars Thomas Ulimwengu (kulia), akijaribu kuwatoka mabeki wa Ivory Coast wakati wa mechi ya kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Dunia, iliyochezwa leo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam               Dar es Salaam,Tanzania
MABAO 4-2 ilitosha kuiondosha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) katika safari ya kwenda  Brazil kwenye mashindano ya Kombe la Dunia,Washambuliaji wa Kimataifa wa Timu ya taifa ya Ivory Coast Yaya Toure, Solom Kalou pamoja na Gervinho waliiwezesha timu yao kuitupa Stars nje ya mashindano hayo.
Stars ndiyo iliyoanza kupata bao la kuongonza kupitia kwa Amri Kiemba akiunganisha mpira nyavuni baada ya mabeki wa Ivory Coast kushindwa kuondoa mpira uliorushwa na Erastal Nyoni.
Wakati watanzania elfu 60 waliokaa kwenye viti vya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wakiendelea kushangilia bao hilo,Ivory Coast wakasawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji Traore Lacina.
Thomas Ulimwengu alipachika bao la pili baada ya kuwashinda nguvu mabeki watatu wa Ivory Coast na kuwainua watanzania kwenye vitu vyao, kufungwa kwa bao hilo ilizidi kuwachanganya miamba hao wa soka kutoka Afrika Magaribi.
Mshambuliaji wa Arsenal Gervinho aliweza kutumia uzoefu wake wakujiangusha na kumfanya Mwamuzi wa mchezo huo Mehdi Abid kutoka Algeria kuizawadia Ivory Coast penalti iliyopigwa na Toure iliyomshinda kipa namba moja wa Stars Juma Kasseja na kufanya matokeo kuwa 2-2.
Ivory Coast waliokuwa wakicheza soka la malengo kutokana na tabia yao ya kufanya mashambulizi makubwa pale wanapofungwa tu walifanikiwa kupachika bao la tatu kupitia kwa Toure aliyepiga mpira wa adhabu ndogo nje ya 18 na kuitinga wavuni.
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Ivory Coast walikuwa mbele kwa mabao 3-2, kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikitafuta ushindi, lakini uzoefu wa mshambuliaji Gervinho iliwashinda mabeki wa Stars na kutoa pasi iliyonaswa na Bonny Wilfred nakupachika bao la nne.

SAKATA LA NGASA KUTO CHEZA JUMAPILI DHIDIYA IVORY COAST



CAF ya mzuia Ngasa kucheza mechi ya Taifa stars na Ivory Coast itakayo chezwa jumapili hii. Kikosi cha taifa stars kitashuka dimbani kesho kutwa kuivaa Ivory Coast katika kuwanini kufuzi kombe la dunia 2014,lakini habari ni kuwa kiungo mshambuliaji Mrisho Ngasa hataa ruhusiwa kucheza kwa kuwa ana kadi mbili za manjano.
Taarifa ambazo championi ijumaa imezipata kutoka ndani ya shirikisho la soka tanzania TFF wamesema wamepokea ujumbe kutoka shirikisho la soka Afrika CAF kwamba ngasa ana kadi mbili za manjano.
Taarifa zina sema kuwa kiungo huyo alipata kadi mbili za manjano katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini wakati stars ikiumana na Morocco wakati mchezo wa kwanza ulio pigwa machi stars ilishinda bao 3-1 kabla ya kupokea kipigo cha 2-1 ugenini.
Tumepoka ujumbe kutoka CAF ju ya Ngassa,nitaarifa ambayo hasa katika ya hizi siku mbili kwa sababu tulikuwa tuna jua kocha alikuwa anajua atakuwa nae katika mchezo wa kesho kutwa alisema kiongozi huyo wa TFF.
Aidha straika wa stars Mbwana Samatta aliema kuwa ile nitimu kama timu nyingine sijaona sababu za kuiogopa au kuihofia tuna asilimia kibao za kuwafunga Ivory Coast ukizingatia tunacheza nyumbani alisema Samatta.

 

MESSI ANATUHUMIWA KWA KUKWEPA KULIPA KODI



Mwanasoka bora wa dunia Lional Messi anatuhumiwa kukwepa kulipa kodi ya kiasi cha 3.4 milioni.Mashtaka yamefunguliwa dhidi ya mshambuliaji huyo wa Barcelona na baba yake ndiye muendesha mashtaka wa kaskikazini mashariki mwa Catalunya mahara ambapo messi ana ishi.

Wote wa wili Messi na Jorge Horacio,wanatuhumiwa kwa makosa matatu kwa kudanganya taarifa juu ya ulipaji wa kodi ambayo inafikia kiasi cha 3.4 milioni cha kodi ya mapato cha mwaka 2007,2008 na 2009.

Jaji katika mahakama ina bidi aya kubari mashtaka ya muendesha mashtaka kabla ya kesi kufunguliwa rasmi.

No comments:

Post a Comment