Sunday, 5 May 2013

MLIPUKO UMETOKEA KANISA KATOLIKI ARUSHA

Hadi sasa Jeshi la polisi linamshikilia mtu mmoja akihusishwa na mlipuko uliotokea katika kanisa la Katoliki Olasiti Arusha

Kwasasa majeruhi wanaripotiwa kuwa 30, ila watu watatu wameumia vibaya sana na hali zao sio nzuri.

RPC mkoa wa Arusha ametoa hotuba yake na kusema ni tukio la kigaidi, pia amesema wanawasaka wote waliohusika na tukio hilo na ameomba watanzania wawe watulivu wakati wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Uzinduzi wa kanisa hilo la Mtakatifu Joseph parokia ya Olasiti umesitishwa hadi hapo utakapotangazwa baadaye.

No comments:

Post a Comment