Saturday, 18 May 2013

HII NDIO TAKWIMU YA SIMBA NA YANGA

Kama haujacheki mpira wa simba na yanga hiki ndio kilichojili uwanjani leo.

shuka nayo hii mtu wangu......

Mpira umemalizika, Young Africans 2 - 0 Simba SC
Kavumbagu ddk 4
Kiiza dkk 63

Dk 85 Nizar Khalfan anapiga shuti kali langoni kwa Simba lakini Kaseja anaokoa na kuumia. Simba 0-2 Yanga

Dk 76 SUB....! Simba imefanya mabadiliko ametoka Haruna Chanongo ameingia Ramadhan Singano 'Messi'

Dakika ya 75, Young Africans 1 - 0 Simba SC
Anaingia Nizar Khalfani kuchukua nafasi ya Hamis Kiiza

Dk 69 Sunzu wa Simba anamchezea faulo Mbuyu Twite wa Yanga. Mpira unasimama kwa muda ili Twite atibiwe.

Dakika ya 63, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la pili - Young Africans 2 - Simba SC

DK 60 Yanga wanaendelea kuongoza hapa dhidi ya Simba

Dk 47 SUB: Simba imefanya mabadiliko, ametoka Abdallah Seseme ameingia Felix Sunzu.

 
Picha zaidi za sherehe za ushindi wa wanajangwani zinakujia hivi punde.
YANGA 2-0 SIMBA

Hatimaye yametimia, kilio kimekwenda Msimbazi baada ya Mabingwa wapya wa Tanzania Bara, Dar Young Africans kuimaliza ligi kwa kishindo kwa kuichapa Simba mabao mawili kwa bila. Mabao ya Didier Kavumbagu katika dakika ya 5 tu ya mchezo huku Hamis Kiiza akipigilia msumali wa pili katika dakika ya 63. Simba watajialumu kwa kushindwa kusawazisha kipindi cha kwanza baada ya Musa Mudde kushindwa kufunga mpira wa dhabu ya penati iliyotolewa na mwamuzi baada ya Mrisho Ngassa kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari.

Picha zaidi za sherehe za ushindi wa wanajangwani zinakujia hivi punde.
Mambo ya mashaka tu.........
Wewe utatupia 'uzi' gani? Mwekundu au wa Kijani? Unatabirije mtanange huu wa watani wa jadi? Je, Yanga italipa kisasi cha 'tano bila'? Je, Simba itaendeleza ubabe kwa Yanga?

#TeamSimba = LIKE
#TeamYanga = COMMENT

Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA!

Mpira ni mapumziko, Young Africans 1 - 0 Simba SC
Dk 38 Simba inapata kona ya pili.
Dk 35 Kiiza wa Yanga anakosa bao la wazi baada ya mpira alioupiga kutoka juu ya lango la Simba. Simba 0-1 Yanga.
Dk 32 Mwinyi Kazimoto wa Simba anamchezea vibaya Frank Domayo wa Yanga.
Dakika ya 28 Simba walipata penati, akapiga Mussa Mudde na kukosa
Dk 27 PENALLLLTTY......! Simba inapata penalti baada ya Cannavaro kumchezea vibaya Mrisho Ngassa.
Dk 21 Hamis Kiiza wa Yanga anauwahi vizuri mpira katikati ya mabeki wa Simba waliojichanganya kuokoa lakini shuti lake hafifu linaokolewa na kipa wa Simba, Juma Kaseja.
Dk 20 Cannavaro wa Yanga anachezewa faulo na Haruna Shamte wa Simba.
Dk 16 YELLOW CARD......! Haruna Shamte wa Simba anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Simon Msuva. Simba 0-1 Yanga

DK 15 Simba 0 - 1 Yanga

Dk 10 Didier Kavumbagu wa Yanga anamchezea faulo Shomari Kapombe.

Dk 8 Simba inapata kona ambayo haizai matunda

Didier Kavambagu anaipatia Yanga bao la kuongoza

Dk 1 YELLOW CARD...! Mbuyu Twite wa Yanga anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Haruna Chanongo wa Simba.

Mpira unaanza uwanja wa Taifa

Simba line up: Juma Kaseja, Nassor Masoud 'Chollo', Haruna Shamte, Shomari Kapombe, Mussa Mudde, William Lucian, Mwinyi Kazimoto, Abdallah Seseme, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba na Haruna Chanongo. Sub: Abel Dhaira, Miraji Adam, Ramadhan Singano 'Messi', Felix Sunzu, Christopher Edward, Jonas Mkude na Hassan Mkude

Yanga line up: Ally Mustapha 'Barthez', Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondan, Athuman Idd 'Chuji', Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Haruna Niyonzima. Sub: Said Mohamed, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nurdin Bakar, Nizar Khalfan, Said Bahanuz na Jerry Tegete.

No comments:

Post a Comment