HAKUNA MLIPUKO WA BOMU KAMA ILIVYOSEMEKANA
Polisi
Mkoa wa Dar es salaam imesema hakuna tukio la ulipoaji bomu katika
Kanisa la KKKT Kunduchi Beach, Eneo la Kunduchi jijini Dar es salaam
kama ilivyovumishwa isipokuwa lilikuwa ni tukio la polisi kupambana na
wahalifu waliokuwa karibu na kanisa na ndipo waliporusha bomu la machozi
kupambana na wahalifu hao,jambo ambalo waumini waliokuwapo kanisa
jirani na eneo la tukio walidhani kuwa bomu limerushwa kanisani.Hii ni
kwa mujibu wa Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam,Suleimani
Kova.
No comments:
Post a Comment