LEO NDIO FAINAL YA UEFA CHAMPION LEAGUE
UEFA CHAMPIONS LEAGUE FINAL:BAYERN MUNICH VS BORUSSIA DORTSMUND NANI ATAIBUKA MBABE WIMBLEY LEO?
MICHUANO ya Ligi ya
Mabingwa barani Ulaya inafikia kilele leo kwa mchezo wa fainali
utakaozikutanisha timu za Ujerumani Bayern Munich na Borussia Dortmund
mtanange ambao utafanyika katika Uwanja wa Wembley jijini London,
Uingereza. Hiyo
ni fainali ya kwanza kabisa kuwahi kuzileta pamoja timu mbili za
Bundesliga katika historia ya michuano hiyo mikubwa kabisa ya vilabu
barani humo. Safari
ya timu hizo kufikia fainali haikuwa rahisi kwani Bayern walilazimika
kuwafunga Barcelona kwa jumla ya mabao 7-0 katika mechi za mikondo
miwili walikutana katika hatua ya fainali huku Dortmund wao wakiizamisha
Real Madrid kwa jumla ya mabao 4-1 matokeo yaliyowashangaza wadau wa
soka duniani kote. Bila
kujali matokeo ya mechi ya leo, bila shaka utakuwa usiku wa kihistoria
kwa soka la Ujerumani, lakini timu hizo mbili zinashuka dimbani zikiwa
na motisha tofauti. Kwa
Bayern, hiyo ni fursa ya kujikomboa kutokana na machungu waliyopata
katika vichapo vya fainali za mwaka wa 2010 na hasa mwaka wa 2012 wakati
walipofungwa na Chelsea kwa changamoto ya mikwaju ya penati, fainali
ambayo ilichezwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Allianz Arena.
No comments:
Post a Comment