wabunge wa chadema wametakiwa kutoisifia serikali iapotekekeza mambo ya maendeleo kwa ufanisi.
Mbunge
wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amewapiga marufuku wabunge wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuipongeza Serikali inapotekeleza
mambo mbalimbali kwa ufanisi ikiwemo miradi ya maendeleo. Akizungumza
bungeni wakati wa Kamati ya Matumzi kabla ya kupitishwa kwa bajeti ya
Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2013/14 Zitti Kabwe mbali na hilo
pia amehoji mahala zilizopo shilingi bilioni 252 zilizotengwa katika
bajeti iliyopita ambazo zimeainshwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) kuwa hazijulikani zilifanya kazi gani. Akitolea
ufafanuzi jambo hilo Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli amesema fedha
hizo zilitumika kulipa madeni ya makandarasi.
No comments:
Post a Comment