Monday, 20 May 2013

MRISHO NGASA ATAMBULISHWA RASMI YANGA

shuka nayo mtu wangu....



Mrisho Ngasa akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu ya Yanga baada ya kutambulishwa rasmi. 
Katibu Mkuu wa klabu ya Young Africans Lawrence Lawrence Mwalusako leo amemtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari mchezaji Mrisho Ngasa ambaye amerejea katika klabu yake ya zamani kufuatia kumalizika kwa mkataba wake wa miaka miatatu (3) dhidi ya timu ya Azam FC.

Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu Mwalusako amesema Ngasa amerejea katika timu yake, alikuwa mchezaji wetu kwa muda mrefu kabla ya kuhamia katika timu ya Azam FC ambako alitumikia mkataba wa miaka 3 uliomalizika mwisho mwa msimu huu.


Pichani ni mchezaji Mrisho Ngasa akisaini Yanga
 JUHUDI za Simba kutaka kuona kiungo Mrisho Khalfan Ngassa anaifunga Yanga juzi zilikwama pamoja na kumuahidi mamilioni ya fedha kama angefunga bao katika mechi hiyo ya watani. Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Simba kulala kwa mabao 2-0, Ngassa aliahidiwa kulipwa Sh milioni tatu kwa kila bao atakalofunga, lakini yeye hakufanya hivyo, badala yake akasisitiza yeye ni “Yanga damu.”

“Simba walimuahidi Ngassa shilingi milioni tatu kwa kila bao ambalo angefunga dhidi ya Yanga, alikubaliana nao lakini akaniambia asingeweza kufanya hivyo kwa kuwa yeye ni Yanga damu,”

No comments:

Post a Comment