Thursday, 9 May 2013

SERIKSLI IMESEMA HAITASAHIHISHA UPYA MATOKEO WALA WANAFUNZI KURUDIA MTIHANI


Serikali imesema haitasahisha mitihani upya wala Wanafunzi kurudia mtihani wa Taifa wa Kidato cha nne wa mwaka 2012, kitakachofanyika ni kurekebisha matokeo yaliyopo kwa kufuata madaraja yaliyokuwa yakitumika miaka ya nyuma wakati wa usahishaji wa mtihani huo.
Akizungumza Jijini Dar es salaam, wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Uboreshaji wa Elimu Tanzania ambao utajikita zaidi katika Lugha ya Kiingereza, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, DK SHUKURU KAWAMBWA amesema Serikali imefikia hatua hiyo baada ya kuona mchakato mpya uliotumika katika usahishaji wa mtihani wa taifa wa Kidato cha nne umewabana sana Wanafunzi.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza, LIZ TAYLOR pamoja na Kamishina wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof EUSTELLA BHALALUSESA wamesema wanaamini mradi huo utachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha kiwango cha Elimu nchini.
Mradi huo ambao utadumu kwa miaka minne unatarajia kugharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 120 huku Wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari pamoja na Walimu ambao wako vyuo mbalimbali vya Elimu ambavyo viko chini ya Serikali wakitarajiwa kunufaika na Mradi huo

No comments:

Post a Comment