JAY Z KUTUA BONGO OCTOBER 4 MWAKA HUU NA ATAPIGA SHOW PALE DAMOND JUBILEE
Tanzania ni miongoni mwa nchi tano za bara la Africa zilizochaguliwa na rapper Sean Carter aka Jay-Z kwaajili ya kutumbuiza kama sehemu ya ziara yake ya wiki saba ya dunia.
Ziara hiyo ni kwaajili ya kutangaza uelewa kuhusu tatizo la maji duniani. Inatarajiwa kuanza September 9 nchini Poland na kuzunguka mabara ya Ulaya, Africa, Asia na kumalizia Australia.
Barani Africa ataanza na show jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee October 4 kisha Accra, Ghana, Lagos, Nigeria, Luanda, Angola, Cape Town, Durban, na Johannesburg, Afrika Kusini.
Source: okayafrica.com
No comments:
Post a Comment