Huyo ndiye Wolper Gambe
BINTI mwenye mvuto kwenye filamu za
Bongo, Jacqueline Wolper, amebadili jina na sasa anataka kuitwa Wolper
Gambe na kusema jina hilo halina uhusiano na kinywaji chochote.“Silewi na si mpenzi wa kilevi, lakini
napenda muziki sana jina langu limetokana na muziki ambao naupenda sana
ndio maana kwa sasa najiita Wolper Gambe ukiniita Wolper Gambe
umefurahisha nafsi yangu kiukweli," alisema."Watu
wanajua eti Gambe ni pombe, hapana hizo ni swaga tu za sisi vijana, kitu
kingine ninachopenda ni kumiliki gari nzuri.”Aidha mwigizaji huyo
alivyoulizwa kuhusu
gharama ya gari yake mpya ya Mini Coper, alisema kuwa gari hiyo ni ya
gharama kubwa lakini hawezi kuitaja gharama hiyo hadharani kwani anaona
itakuwa kama kuwakejeli wengine."Unajua kuna watu hawawezi hata kumiliki
fedha ya kununulia chakula kidogo tu, sasa katika mazingira hayo kutaja
thamani kubwa ya gari ni dhihaka kwa wengine," alisema.
No comments:
Post a Comment