Wednesday, 15 May 2013
NGASA AWEKA SAINI YANGA
KIUNGO mwenye kasi, Mrisho Khalfan Ngassa, amerejea Yanga na kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea tena timu hiyo.
Ngassa alianza kupata umaarufu mkubwa akiwa na Yanga kabla ya kuondoka na kujiunga na Azam FC kwa kitita cha jumla ya Sh milioni 98 na kuweka rekodi mpya ya usajili.
Lakini Ngassa ameamua kusaini tena mkataba wake mpya Yanga wakati akiwa chini ya klabu ya Simba ambao ni watani wakubwa wa Yanga.
Simba na Yanga zinakutana Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment