Friday, 10 May 2013

TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012

*Mnamo tarehe 03 Mei, 2013 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Wiliam Lukuvi (Mb) ilitoa Kauli ya Serikali Bungeni Kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Sababu za kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka 2012. * * * *Kauli ya Serikali ilielekeza kuwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012 yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011 ili Wanafunzi hao wawe katika mazingira yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita kwa kuwa mfumo uliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule uliotumika mwaka 2011 na miaka mingine iloyopita.Kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume na maelezo la balaza la mawaziri, waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi kwa mamlaka aliyonayo chini ya sheria ya Balaza la Mitihani Tanzania kifungu namba 20 sura 107 ameliagiza Balaza la Mitihani la Taifa kupitia upya matokeo ya mitihani ya kitado cha nne mwaka 2012 aidha ameagiza kupitia upya matokeo na sio kufanya tena mtihani huo.

 

No comments:

Post a Comment