Thursday, 23 May 2013

KAULI YA RAISI DHIDI YA VURUGU YA MTWARA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo Dodoma,Tanzania
WAKATI hali ikizidi kuwa tetea Mkaoni Mtwara kufuatia Mapigano yaliyoanza jana Mkoani humo Rais Kikwete amevunja ukimwa wake na kutoa amri  wahusika wakuu wa tukio hilo kusakwa mara moja.
Akizungumza katika eneo la Kizota, Dodoma wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Dodoma kwenda Iringa, Rais Kikwete
alisema wote waliohusika na vurugu hizo watasakwa na kuchukuliwa hatua kali.

Rais Kikwete alisema rasilimali inayopatikana mahali popote pale nchini inatakiwa kutumiwa na Watanzania wote... “Hivi watu wa
Nyarugusu wadai dhahabu ya pale au kinachopatikana Chalinze basi kisitumiwe na watu wa Morogoro! Hivi tutakuwa na taifa kweli?,”
alihoji kwa ukali Rais Kikwete.

Rais Kikwete alisisitiza kuwa Serikali itawasaka wale wote wanaoongoza vurugu hizo na watawajibishwa kwa makosa hayo... “Tutawasaka
hawa watu na viongozi wao hata kama wana mapembe kiasi gani, tutayakata.”

Kwa upande wake Waziri Muhongo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisoma taarifa ya mapato na matumizi ya Wizara yake alisema mradi wa kusafirisha gesi kutoka mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam,  umeanza kwa kasi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakwenda huko wiki ijayo kuweka jiwe la msingi. Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini jana, Waziri Muhongo alisema:
“Mradi wa kujenga bomba la gesi uko palepale na unaendelea kwa kasi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ataenda kuweka jiwe la msingi wiki
lijalo.” “Tumezungumza mengi kuhusu suala hilo na hata viongozi wa watu wa Mtwara walipelekwa nje kujifunza faida zake, lakini hata kama  hawajaelewa, nimetoa kijitabu kinachozungumzia faida mbalimbali watakazopata wana Mtwara katika mradi huo.

No comments:

Post a Comment