Friday, 31 May 2013

WADADA WAWILI WA KIPAKISTAN WAFUNGA NDOA YA JINSIA MOJA

HAWA NDIO WADADA WALIO FUNGA NDOA YA JINSIA MOJA

Mashoga hao wakifungishwa ndoa kwenye ofisi ya msajili nchini Uingereza.
Wanawake wawili raia wa Pakistan wameweka historia kama Waislamu wa kwanza wa jinsia moja kufunga ndoa nchini Uingereza.

Rehana Kausar, miaka 34, na Sobia Kamar, miaka 29,wameweka historia pale walipofunga pingu za maisha katika sherehe iliyofanyika kwenye ofisi ya msajili, kisha haraka wakaomba hifadhi ya kisiasa baada ya kuwa wamefunga ndoa, wakidai kwamba maisha yao yatakuwa hatarini kama wakirejea kwenye nchi yao ya asili.
Wakishuhudiwa na wasimamizi wao na marafiki wawili, wanandoa hao walivalia mavazi meupe asilia ya ndoa pale walipofunga ndoa mjini Leeds, West Yorkshire.
Wawili hao, kutoka mikoa ya Lahore na Mirpur ya Pakistan, walisema walipokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa wapinzani nchini Pakistan - ambako mahusiano ya jinsia moja ni kinyume cha sheria na kuchukuliwa ni kusaliti Uislamu.
Na tangu habari za ndoa yao mapema mwezi huu kuzagaa, wanandoa hao walidai kupokea vitisho vya kuuawa hata kutoka nchini Uingereza 
Kabla ya zoezi hilo, hata msajili aliwashauri wawili hao kufikiria kwa makini kuhusu uamuzi wao wa kufunga ndoa sababu ya mtazamo wa baadhi ya Waislamu kuhusu mahusiano ya jinsia moja.

Kausar alisema: "Nchi hii inatupatia uhuru wa kuamua na ni uamuzi binafsi mno ambao tumeuchukua.
"Halimuhusu mtu mwingine yeyote kwa hili tunalofanya katika maisha yetu binafsi.
"Tatizo lililopo Pakistan ni kwamba kila mmoja anaamini ni nyapara wa maisha ya watu wengine na anaweza kuamua vema kuhusu imani za watu wengine lakini huo si mtazamo sahihi na tupo katika taifa hili sababu ya makasisi wetu ambao wameteka nyara jamii yetu ambayo ni jamii vumilivu na inayoheshimu uhuru wa watu binafsi."
Kamar, alimwelezea mpenzi wake kama 'mwenza wa kiroho' na alisema wanawake hao wawili walizama kwenye mapenzi.
Sheria za Pakistan hazitambui ndoa za jinsia moja na hakuna sheria kukomesha ubaguzi.
Wanawake wote walikutana mjini Birmingham kama wanafunzi ndipo wakahamia nchini Pakistan kutoka Uingereza.
Baadaye walianza kuishi pamoja kama wapenzi huko South Yorkshire, ambako walikaa mwaka mmoja kabla ya kuamua kufunga ndoa.
Jamaa mmoja alisema: "Wapenzi hao hawakuwa na ndoa ya Kiislamu, inayofahamika kama 'nikah', kutokana na kushindwa kumpata Imamu wa kuendesha kile kinachoonekana kama ndoa yenye utata.
"Wamekuwa majasiri wakati wote kutokana na dini yetu kukataza mahusiano ya jinsia moja.
"Wanandoa hao wamekuwa wakitishiwa maisha kote hapa na Pakistan na hakuna namna yeyote wanayoweza kurejea kule."
Wanafunzi wengi wa Sharia - Sheria ya Kiislamu wanatazama mahusiano ya jinsia moja kama ni dhambi inayostahili adhabu kali.

K.LYNI AMEMTAJA REGINALD MENGI NDIYE BABA WA MAPACHA WAKE

Hatimaye Miss Tanzania 2000 amtaja REGINALD MENGI kuwa ndiye baba halisi wa watoto wake mapacha angalia hapa alichokiandika katika ukurasa wake wa Twitter.shuka nayo hapa mtu wangu.......

 
clip_image001clip_image002

NEWZ:AJALI YATOKEA BAADA YA KUJARIBU KUDANDIA DALADALA

Afariki baada ya kuanguka akidandia daladala, Dar

afariki-akidandia-daladala-0
afariki-akidandia-daladala
Mtu mmoja ambaye jina lake bado halijafahamika, amefariki dunia baada ya kuteleza na kuanguka wakati alipokua akijaribu kudandia Daladala maeneo ya Ilala Boma, Jijini Dar es Salaam, asubuhi leo. Marehemu huyo baada ya kuanguka na kupiga kichwa kwenye lami, alipasuka kichwa na kuvuja damu nyingi kichwani, na kufariki katika eneo la tukio.

Mwili wa marehemu umepelekwa katika Hospitali ya Amana, Ilala.
 Wasamaria wema wakisaidia kumpakia kwenye gari kwa kumpeleka hospitalini
                
Damu ya marehemu ambayo kwa kiasi kikubwa imetoka kichwani baada  ya kupasuka vibaya
Mwili wa marehemu ukiwa tayari kuondolewa kwenda hospitali
               
Hii ndio daladala ambayo marehemu alikuwa akitaka kudandia na kudondoka kwa bahati mbaya
Umati wa watu ukishuhudia ajali maeneo ya Ilala Boma asubuhi hii
                                   

Thursday, 30 May 2013

HAYA NDIO MATUKIO YANAYOENDELEA HUKO AFRIKA KUSINI

Yanayoendelea huko Afrika kusini katika hospitali ulipo mwili wa marehemu Albert Mangwea

Muonekano wa nje wa hospitali ya St Hellen Joseph, ulipokuwa mwili wa marehem Albert Mangwea

Millard akifanya mahojiano na mmoja wa watanzania walioko Soth Africa

Nje ya mochwari ya Serikali Hillbrow Johannesburg ulikohamishiwa mwili wa Ngwea ni Watanzania wakiongozwa na Kinje Ngomale Mwiru wakitazama sample ya majeneza mbalimbali ili wajue la kununua, hapa walikua na mfanyabiashara wa kampuni ambayo pia huwa inashughulika na kusafirisha miili ambapo gharama yake ni zaidi ya milioni nne na nusu.



Millard Ayo akifanya interview na mmoja wa Watanzania nje ya hospitali alikolazwa M2TheP.
source: clouds fm

MATOKEO MAPYA YA KIDATO CHA NNE HADHARANI

Wazri wa elimu Dr Shukuru Kawambwa anatangaza matokeo mapya ya kidato cha nne kaa mkao wa kula kupata matokea yako........

SIKILIZA KAULI YA DIAMOND KWENYE TAKE ONE YA CLOUDS TV

Diamond afunguka kuhusu Wema, Penny, Jokate, Uwoya, Aunt katika “Take One”

diamond-zamaradi-mketema-wema-sepetu

diamond-zamaradi-mketema-wema-sepetu-0

Msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefunguka kupitia kipindi cha Take One cha Clouds TV, kuwa hana tena mapenzi na aliyekuwa mpenzi wake, mrembo Wema Isaack Sepetu. Akihojiwa na Zamaradi Mketema katika kipindi hicho, Diamond ameeleza anavyomfeel sana mpenzi wake wa sasa Penny ambaye anadai anamuheshimu na wala hamcheat.

Kuhusu kutoka kimapenzi na wasanii wa Filamu Bongo, Irene Uwoya pamoja na Aunt Ezekiel, Diamond ameruka kwa kusema kuwa anamheshimu sana Uwoya wakati akidai kuwa Aunt alikuwa demu wa mshikaji wake.
Mkali huyo ameweka wazi pia kuhusu mapenzi yake na Jokate kwa kummwagia sifa kadhaa na kueleza kuwa yeye ndiye mwenye makosa maana Jokate alikuwa innocent na hakuwahi kumkosea japo aliachana naye na kurudi kwa Wema kabla hajaangukia kwa mrembo Penny ambaye ndiye anataraji awe mama watoto wake.

ANGALIA HAPA MAMA LULU, MAMA KANUMBA NA LULU KWENYE SHEREHE YA PAMOJA

Picha zote zipo hapa..........
mama lulu na mama Kanumba wakicheza
kwa pamoja
lulu akicheza na mama zake
 katikati ni lulu akiwa na mama zake
happy people
tunakula bata mpaka kuku anaona wivu

Wednesday, 29 May 2013

M 2 THE P ALIYEKUA NA MAREHEMU NGWAIR BADO YU HAI

  HIZI NDO HABARI ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE..

Albert Mangwea 'Ngwair' na M to the P
Kumekuwepo na sintofahamu kuhusu hali ya msanii M To The P ambae alikuwa rafiki wa karibu wa marehemu Albert Mangwea a.k.a Ngwair, msanii huyu inasemekana alikuwa na marehemu wakitumia pombe kali na madawa ya kulevya na kujikuta wanazima wote katika chumba kimoja na kukimbizwa St.Hellen Hospital ambapo umauti ulimfika Ngwair.

Kwa kuwa ripoti zinapatikana kutoka Afrika kusini na wachache sana ndio wenye mawasiliano ya moja kwa moja na watu walioko hospitalini hapo na hadi sasa hakuna mzungumzaji maalum aliyeteuliwa kutoa taarifa kutoka hospitalini hapo, inaweza kuwa chanzo cha habari kutofautiana.

Kwa waliosikiliza TBC Taifa saa kumi katika kipindi cha ‘harakati’ wametangaza kuwa M to the P amefariki dunia asubuhi ya leo na mipango ya kusafirisha miili ya wawili hao inaendelea.

Lakini habari za uhakika zilizopatikana ni kwamba msanii huyo bado yuko hai japokuwa hali yake ni mbaya sana.

Msanii Bushoke na baadhi ya ndugu wa marehemu tayari wako Afrika kusini na ripoti zilizopatikana kutoka kwao zinasema msanii M to the P anaendelea vizuri, japo alikuwa anapumulia mashine alipowaona alipata nguvu akanyanyuka kidogo akiwa pale pale kitandani.

Millard Ayo mtangazaji wa kipindi cha amplifaya cha Clouds Fm ambae yuko katika hospitali ya St. Hellen Johannesburg, amethibisha kuwa M to the P yuko hai. Hii ni tweet yake muda mfupi uliopita.

“#BREAKING Sio kweli kwamba m2theP kafariki, ni mzima ila anapumulia mashine, kafungua macho na kunyanyua miguu dakika chache zilizopita.”

Watanzania waliofika hospitalini hapo wamepata nafasi ya kuuangalia mwili wa marehemu na wanasema walikuwa nae hadi jana majira ya saa kumi jioni, inasikitisha sana.

Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu bado inaendelea.

TARAJIA KUPATA WIMBO WA DIAMOND NA CHEGE HIVI KARIBUNI

Picha zote hizi hapa zikionyesha Diamond na Chege wakiwa studio wakirekodi...........




wakiteta jambo


Diamond With Qboy Mnyama

Diamond na wasafi Photographer goes by the
name Kisula......
akisikiliza demo baada ya kumaliza kufanya
Nusu ya nyimbo hii.....

huyoo ndio Diamond bwanaa...

TAARIFA YA NURSE KUJARIBU KUMTOA MIMBA MWANAFUNZI

Mwanafunzi akiwa kitandani tayari kwa kutolewa mimba

MUUGUZI wa kike, Violet Shoo, mkazi wa jijini Dar ametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi Kituo cha Buguruni, Ilala baada ya kunaswa katika jaribio la kutaka kumchoropoa ujauzito msichana mmoja aliyepandikizwa kama mwanafunzi kwa mtego makini ulioratibiwa na Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’

Tukio hilo lilitokea Jumamosi ya wiki iliyopita, saa 11 jioni kwenye zahanati iliyopo Tabata Matumbi, jijini Dar es Salaam. 
 Nesi akidhibitiwa na polisi...

Muuguzi huyo alikutwa ndani ya zahanati hiyo akiwa na zana mbalimbali zinazodaiwa ni za kutolea mimba huku msichana huyo akiwa juu ya kitanda, tayari kwa kufanyiwa zoezi hilo haramu.
 
Awali, Ijumaa ya Mei 23, mwaka huu baadhi ya wakazi wa eneo hilo walitutumia ujumbe  wakimlalamikia muuguzi huyo kwamba amekubuhu katika matukio ya utoaji mimba hivyo wakaomba ikiwezekana OFM imuandalie mtego wa kumnasa ili kukomesha kitendo hicho.
 
“…huyu nesi amekuwa akiwatoa watoto wetu mimba, kwa siku anaweza kutoa hadi nne, sisi wazazi tumechoshwa, tunaomba mje. Anaitwa Violet…” ilisomeka sehemu ya meseji hiyo huku ikielekeza zahanati anapopatikana.
Nesi akiwa chini ya ulinzi....
Baada ya malalamiko hayo, kikosi cha upelelezi cha OFM chenye wasichana wawili kilikwenda kwenye zahanati hiyo na kukutana uso kwa uso na muuguzi huyo ambapo msichana mmoja aliomba kutolewa mimba na nesi huyo ambapo aliambiwa ni shilingi 50,000.

Kikosi kiliondoka kwa kumwambia muuguzi huyo kwamba wanafuata fedha mahali na wangerejea jioni wakiwa na  pesa mkononi. 

Timu ya waandishi wetu wa habari  pamoja na Jeshi la Polisi waliweka mtego baada ya wakazi wa maeneo iliyopo zahanati hiyo kulalamika juu ya kukithiri vitendo vya utoaji mimba vinavyofanywa kwa muda mrefu na muuguzi huyo.
 
Wakazi wa maeneo hayo ambao hawakupenda majina yao yaandikwe , walidai kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na kupiga simu katika chumba cha habari kuwa idadi kubwa ya wanawake wanatolewa mimba kwa siku katika zahanati hiyo bubu ambayo haina jina wala hadhi ya kutoa huduma.
 
Baada ya hapo, waandishi hao wa kike walirejea ofisini na kutoa taarifa kwa mabosi wao ambapo timu kamili ilipangwa.

Mkuu wa timu hiyo alianzia Kituo cha Polisi Buguruni ambapo alitoa taarifa kuhusu malalamiko ya wakazi wa eneo hilo na jinsi muuguzi huyo alivyofikia hatua ya kutaka alipwe elfu hamsini ili kukamilisha zoezi.
 
Afande mkuu akatoa maagizo kwa watu wa chini yake watatu, akiwemo askari wa kike mmoja kwa ajili ya kwenda kumnasa nesi huyo.

Msichana aliyepandikizwa kutolewa mimba akiwa na mwenzake walitangulia kufika kwenye zahanati hiyo lakini hawakumkuta muuguzi huyo. 
Mfanyakazi mmoja wa zahanati hiyo alimweleza ‘mtolewa mimba’ kwamba nesi huyo alikwenda kusuka na tayari ameshawasiliana naye hivyo wasubiri.

Saa kumi na nusu, muuguzi huyo aliwasili kwa ajili ya kazi hiyo huku mawasiliano yakifanyika kati ya mtolewa mimba na waandishi waliokuwa jirani na eneo la tukio.
 
Ndani ya dakika kumi, waandishi na polisi waliitwa eneo la tukio wakijulishwa kwamba ‘mjamzito’ huyo ameshavua nguo tayari kwa kazi ya kuchoropolewa mimba.

Kikosi kazi kilivamia zahanati hiyo ambapo walikuta zoezi linaendelea. Polisi wenye ujuzi wa kazi za kunasa matukio walimtia mbaroni muuguzi huyo akiwa na zana za shughuli huku wakimwambia kosa lake.
Vifaa vinavyotumika katika kutoa mimba......
 
Wakati huo, mjamzito alikuwa yupo kitandani katika maandalizi ya kutolewa mimba.

Wananchi waliokuwepo eneo la tukio wakati mtanange ukiendelea, walionekana kufurahishwa na kitendo cha kukamatwa kwa muuguzi huyo huku wakidai walikuwa wamechoka naye kutokana na vitendo vyake vya kutoa mimba hadi kwa wanafunzi.

NEWS: TAARIFA KUHUSU MAZISHI YA NGWEAR

TAARIFA YA KIFAMILIA KUHUSU MAZISHI YA NGWEA NA JINSI MWILI HUO UTAKAVYOLETWA TANZANIA

 
Baba Mdogo wa Marehemu Mzee Mangweha ambaye yuko Mbinga Songea kikazi, amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake mkubwa yaani baba mkubwa wa Ngwair, David Mangweha ambaye naye yuko Songea kuwa watu watakutanika Mbezi kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika hapa Dar es salaam Mbezi Beach. 
Ingawa bado kikao cha familia nzima hakijafanyika lakini baba huyo mdogo amesema wanaweza kulazimika kuzika Morogoro sehemu ambayo baba yake alizikwa.
Baba huyo mdogo alisema kuwa kesho ndo watarudi Dar es Salaam pamoja na kaka yake yaani baba mkubwa wa marehemu. 

Kuhusu mwili kuletwa hapa Tanzania kutoka Afrika Kusini baba mdogo amesema kuwa mpaka sasa hawajajua jinsi gani mwili huo utafika hapa lakini kuna ndugu zao ambao tayari washaanza kufanya taratibu za kuwasiliana na ubalozi wa Afrika Kusini ili kujua ni jinsi gani mwili huo utafika hapa.

Kama kutakuwa na mabadiliko yeyote watakapowasili kesho baba mdogo na baba mkubwa baada ya kikao cha familia watatoa taarifa.

Tuesday, 28 May 2013

MSANII MANGWEA AMEFARIKI DUNIA

Breaking Nyuzzzz: Msanii wa Bongo Fleva,Mangwea afariki dunia

 

ripoti kamili
Taarifa Nilizo Pata Kutoka South
Africa Kutoka Kwa Hussein
Original Ambaye Yupo Pretoria
Amesema Ngwear Amefariki Leo

Asubuhi. Alikuwa Ghetto Moja Na
Msanii M To The P.
Walivyokwenda Kuwagongea
Asubuhi Walikuta Ngwear
Amefariki Na M To The P
Amepoteza Fahamu Kabisa. Pia
Daktari Ameshatoa Taarifa Kwa
Watu Wa Karibu Wa Ngwear
Huko South Africa. Ngwea akiwa na msanii M to the P jana south africa.mtu wa karibu anasema walitakiwa kurudi dar leo lakini waliwakuta wamezima kwenye room wote wawili baada ya kuji overdose madawa ya kulevya na M to the P yupo hoi hospitali.

Adamu Mchomvu Akanusha Kuhusika na Status ya Facebook iliyopostiwa Kwenye Account yake Kuhusu Picha za lady Jay Dee

story nzima hii hapa.............

 Baada ya Account ya Adamu kuandika Status kuhusu picha chafu za lady Jay Dee Muda mchache ulio pita Ameandika Status hii Hapa chini :

"Naomba kuchukua nafasi hii kuomba radhi kwa yeyote aliyekwazika kwa maneno machafu yaliyoandikwa kwa wall yangu, na pia naomba nieleweke kwamba sihusiki na chochote kupost au kuandika chochote kuhusu kikwete foundation na picha za jdee ukiwa naked, sina ugomvi na yeyote naheshimu hisia za kila mtu nikiamini kila mtu Anamaamuzi yake.. Aliyeamua kutumia jina langu kufanya hao najua sasa unajiskia vizuri baada ya matusi mengi niliyotukanwa.. Maisha hayaishii hapa siku zinaenda na ukwali utafahamika siku moja ... Mchana mwema !!"

HUU NDIO ULINZI ALIONAO MSANII JAGUAR WA KENYA

Msanii Jaguar Kutoka Kenya anae fahamika kupitia Nyimbo Kama Kigeugeu na Kipepeo Amesema ulinzi alionao kwa sasa unamsaidia kufanya mambo yake vizuri zaidi. Walinzi wanaharakisha mambo na kumuweka salama muda wote anapokuwa kwenye issue zake. Jaguar amesema muda mwingine anazungukwa na mashabiki kitu ambacho anapenda ila sio kila mtu ni shabiki wake pia humu kuna madui na watu wasiompenda. Chochote kinaweza kutokea kwake sababu yeye ni mtu maarufu kama msanii au mwana siasa pale Kenya. Na Swali kama ni walinzi wake , Jibu Ni Yes Ni Walinzi anao watumia akiwa kwenye shughuli kubwa zenye watu wengi.
pichani katikati ni Jaguar