Dar es Salaam. Ulinzi katika ziara ya Obama ni wa hali ya juu kuliko
ulinzi wa aliyewahi kupewa Rais yeyote wa Marekani kwa safari yake ya
Afrika mwaka huu.
Tayari jeshi la nchi hiyo limewasili nchini, kuweka mambo sawa na
kukagua maeneo yote ya karibu na sehemu atakazotembelea na kupita wakati
wa ziara hiyo. Maaskari na majasusi zaidi ya 500 wapo Dar es Salaam
kuhakikisha usalama huo na kuweka vifaa mbalimbali vya mawasiliano
Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam.
Licha ya hilo, ziara yake kutakuwa na askari 1,687 wakataokuja kwa meli
maalumu kubwa ya kivita iliyosheheni silaha mbalimbali, ikiwamo ndege
sita za kivita aina ya AV-8B Harrier na helikopta za kivita 23, ambazo
zinatarajiwa kupasua anga la Tanzania kuimarisha ulinzi.
Meli hiyo ya kisasa aina ya Wasp Class (Uk 1), pia itakuwa imebeba meli
nyingine zaidi ya tano maalumu kwa kubeba vifaru, magari ya deraya,
askari na vifaa vingine itatia nanga Bahari ya Hindi kuongeza nguvu
iwapo lolote litatokea.
Taarifa inaonyesha italazimika kuwapo kwa meli tatu za aina hiyo wakati
wa ziara yake nchini Senegal, Tanzania na Afrika Kusini kwani mwendo
wake siyo kasi hivyo kulazimika kutumia zote hizo kwa ajili hiyo.
Meli hiyo kubwa imeundwa kuwezesha askari wa Marekani kuingia kwa
urahisi eneo la vita kwa brigedi nzima, kwani wanaweza kutumia aina zote
za vita majini, angani na ardhini. Ni meli aina hiyo zilizotumika vita
vya Marekani na Iraq. Licha ya mitambo ya kivita, ina hospitali kubwa
yenye uwezo wa kulaza zaidi ya wagonjwa ya 600.
No comments:
Post a Comment