Usiku wa Tuzo za Muzizki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Tanzania
Music Awards 2013 unatarajiwa kuonyeshwa live mtandaoni siku ya
Jumamosi, Juni 8. Tofauti na miaka mingine ambayo tukio la utoaji tuzo
tu ndio lilikuwa likionyeshwa kupitia kwenye TV pekee, na kuwanyima
fursa Watanzania waishio nje ya nchi kufuatilia moja kwa moja, mwaka huu
watumiaji wa mtandano waka mwanzo tu Internet wataweza kuangalia tukio
la Red Carpet litakaloanza saa moja jioni wakati wanamuziki na wageni
waalikwa wakiwasili ukumbini.
Pia tukio la utoaji tuzo litakaloanza rasmi saa tatu usiku litakuwa
moja kwa moja mtandaoni hadi litakapofikia mwisho. Watumiaji wa simu za
Android, Blackberry, iPhone na tablets wanaweza ku-download application
ya LIVESTREAM itakayowawezesha kuangalia moja kwa moja kwenye simu zao
wakati watumiaji wa computer watatazama kupitia http://new.livestream.com/KTMA2013 na katika Blogs mbalimbali.
Pia picha za matukio yatakayokuwa yakijiri ukumbini zitapatikana
kupitia ukurasa wa Instagram wa kilimanjaro Premium Lager ambo ni www.instagram.com/kili_lager wakati ule wa Twitter www.twitter.com/kili_lager
utakuwa ukitoa habari zinazoendelea na washindi wa tuzo na itapatikana
pia katika ukurasa wa Facebook wa Kilimanjaro Premium Lager.
No comments:
Post a Comment