Wednesday, 12 June 2013

ANGALIA PICHA ZA LWAKATALE ALIVYOPATA DHAMANA JANA


Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare akiingia katika chumba cha ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, kabla ya kupata dhamana katika kesi yake inayomkabili ya kula njama ya kutaka kumzuru kwa sumu Mhariri wa gazeti la wananchi.

Wilfred Lwakatare akiwa na furaha pamoja na wakili wake baada kupata dhamana katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni mshtakiwa wa pili katika kesi inayomkali akiwa amerudi rumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti ya dhamana.
Wakili wa Wilfred Lwakatare, Peter Kibatara akiwa katika picha ya pamoja na mteja wake Wilfred Lwakatare pamoja na wadhamini wake muda mfupi baada ya kuachiwa kwa dhamana na mahakama leo.
Baada ya kupata dhamana safari ya kuelekea uraiani ilianza.
Lwakatare akipandishwa katika Pickup.
Akiwashukuru wanachama na wafuasi wa chama chake.
Msafara ukiondoka katika maeneo ya Mahakama.
Wafuasi wa Chadema wakiwa nje ya Mahakama ya Kisutu.
Ulinzi pia ulikiwa mkali

No comments:

Post a Comment