Monday, 24 June 2013

RAIS WA SOUTH AFRICA JACOB ZUMA ATHIBITISHA KUWA HALI YA NELSON MANDELA NI MBAYA


Hali ya Rais wa Kwanza South Africa Mzee Nelson Mandela
Imezidi kuwa tete baada ya siku ya jana usiku kulala bila kufumbua
macho....


Rais wa wa sasa wa South Africa Jacob Zuma alizungumza kulitangazia Taifa na
Dunia nzima kuhusu hali ya Mzee Mandela.....
"Zaidi ya madokta 20 wanafanya kila wawezalo kufanya kila njia ili hali ya
mzee wetu irudi kama zamani,Ingawa hadi sasa madaktari awajasema lolote
baada ya tukio la jana la siku nzima kutokufungua macho.....
Akizidi kuzungumza Zuma alisema''Madiba ni mgonjwa hospitalini
sana ni baba wa Taifa ili na ni mtu aliepigania uhuru wa nchi hii,
alifungwa miaka 27 kutafuta Uhuru wa nchii hii na Amani....
Ni mtu mzima na umri umeenda sana kwake na kutokana na umri wake
hali yake nayo inazidi kuzorota....Inatupasa wananchi wote na
Dunia nzima kumuombea mzee mandela kwa Mungu juu ya hali yake..''
Akizungumza tena Msemaji kutoka Ofisi ya Rais Ndugu
Mac Maharaj''Aitowezekana kutoa taharifa kwa sasa juu ya chochote
lakini kutokana na Familia watatoa tamko nakueleza kila kinachoendelea
kwa sasa ni sala zenu zinahitajika kumuombea baba wa Taifa ili...''
Alisema msemaji wa Rais.......

Mandela ambae alikuwa Rais wa South Africa baada ya kufungwa Miaka 27
jela kipindi cha ubaguzi wa Rangi nchini humo mwaka 1994...
Ikumbukwe Mandela amelazwa tokea June 8 mwaka huu na leo ni siku
ya 17 toka awepo hospitali kutokana na kuwa na matatizo ya mapafu....
Hii ni mara ya 4 Mandela kulazwa hospital tokea December mwaka jana...!!

No comments:

Post a Comment