Friday, 7 June 2013

RASIMU MPYA MAANDAMANO RUKSA

Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal,akionyesha rasimu ya katiba
WAKATI  vyombo vyadola vikizidi kuwa kero kwa wananchi wanaohitaji kuandamana badala ya kuwalinda kwa muujibu wa katika ya sasa,rasimu ya Katiba Mpya imependekeza haki ya kuandamana na kueleza wazi kwamba raia wanayo haki ya kuandamana kwa amani bila kizuizi.
Rasimu hiyo imeleza kwa uwazi kwamba "utakuwa wajibu wa Mamlaka ya dola kuhakikisha kuwa raia wanapoandamana kwa amani hawabugudhiwi, na kunyanyaswa na vyombo vya usalama".
Kuhusu haki ya kutoa maoni na habari rasimu hiyo imeweka bayana kwamba Kila mtu anao uhuru wa kuwa na mawazo yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea au kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati tofauti ya Katiba ya sasa inavyoeleza na kuminya uhuru huo hususan kwa vyombo vya habari.
Rasimu hiyo imeleza wazi kwamba Kila mtu anayo haki ya kupewa taarifa za matukio mabalimabali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za binadamu na pia taarifa kuhusu masuala muhimu kwa jamii.

No comments:

Post a Comment