Huyu mama alikaa juu ya paa kwa siku
tatu tangu jumamosi kupinga nyumba yao kuchukuliwa na bank.Anasema
mumewe alimdhamini mtu alipochukua mkopo bank miaka mingi iliyopita na
kushindwa kulipa mkopo huo.
Kwa mujibu wa maelezo yake kesi yao bado ipo mahakamani kwani tayari yule mdaiwa kuna mali zake zilizotaifishwa.
Mdaiwa alikopa ml 240 wameuza nyumba
zake 2 na mabasi mawili.Wenyewe wanachodai katika hilo deni imebaki tsh
ngapi na wao watoe?kama nyumba iuzwe watoe deni la bank na hela
inayobaki wabaki nayo wao.
Nyumba ipo mbezi Tangi bovu na
inaeneo kubwa sana mama anasema hata akiuza si chini ya ml 500 iweje
atolewe kwa ml 240?wakati mdaiwa nyumba zake mbili zimeshachukuliwa na
mabasi mawili yale makubwa ya safari za mikoani.Hiyo ml 240 haijatimia
tu?na kama bado kiasi gani kimebaki?
Ndani
ya nyumba vitu walishachukua hao watu wa auction mart ndani kweupe.Na
wakati haya yakiendelea hakukuwa na amri yoyote iliyotoka mahakamani
wala hawakuwa na kibali cha mahakama.
Gea alimfata huko huko juu kumsikiliza na tumemsikia leo kwenye heka heka.Kesho pia itaendelea.
Hapa mabaunsa wakimfukuza
Wamemshika
Wamempa kanga nyingine 2 ajifunge maana hakuwa na nguo zaidi ya hiyo kanga moja.
Eneo la nje kulivyokuwa
Nje ya geti la hiyo nyumba
Chumba cha habari cha clouds fm kimeenda kufatilia hapo bank ya Tanzania Investment bank(TIB)kujua kulikoni??
Maana wakati haya yakiendelea hiyo
jana inasemekana hii nyumba imeshauzwa.Inauzwaje na shauri lipo
mahakamani?Na jana mume wa huyu mama alikuwa mahakamani maana ilikuwa
siku ya kesi kuendelea kusikilizwa.
Na mumewe alirudi na oda maalum kutoka mahakamani kuwa nyumba hiyo isiguswe na vitu vyao virudishwe.A
Chanzo:Dina Marios
Chanzo:Dina Marios
No comments:
Post a Comment