Thursday, 13 June 2013

MBUNGE WA MTWARA HATIMAYE APEWA DHAMANA YA KESI YAKE

stoty yote iko hapa...


Mbunge wa jimbo la Mtwara mjini kupita tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Hasnein Murji aliye achiwa baada ya kutimiza masharti ya liyo tolewa na mahakana na kumuwezesha kuwa huru kwa Dhamana.
Mbunge huyo alirudishwa Rumande juzi kutokana na kuto timiza masharti sharti hilo lilikuwa ni kuwa na Hati ya kusafiria ambayo aliiacha Dar es salaam.
Hakimu mkazi mfawizi mkoa wa Mtwara, Dynes Lyimo alimuachia mbunge huyo kwa dhamana na kumtaka mtuhumiwa na mdhamini wake kusani hati za kumtolea dhamana.
Baada ya maelezo yote hakimu Lyimo aiahilisha kesi hadi Julai 4 mwaka huu mahakamani hapo.
Mbunge huyo alifikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani hapo mwishoni mwa wiki akituhumiwa kwa uchochezi anao daiwa kufanya Januari19 mwaka huu eneo la Ligula mkoani hapo.
Hata hivyo viongozi wengine wa vyama vya upinzani wana husishwa na vurugu za gesi wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa mara nyingine kesho kusikiliza kesi inayo wakabili yenye makosa matatu.
Viongozi hao ni Katani Ahmed Katani mwenye miaka (33)na Said Kulanga mwenye miaka (45) wa chama cha CUF,Hassan Uledi mwenye miaka (35) wa NCCR Mageuzi na Hamza Licheta mwenye miaka (51) wa TLP wote wakazi wa mkoani Mtwara.
Mbunge huyo pamoja na wenzake hao wanashtakiwa kwa makosa ya uchochezi yaliyo pelekea kufanyika kwa vurugu na kusababisha uvunjifu wa amani na mali za watu pamoja na miundombinu kuharibiwa vibaya. 

No comments:

Post a Comment