Wednesday, 12 June 2013

KAMATI KUU YA CCM YAPOKEA CHINI YA MWENYEKITI DK. JAKAYA KIKWETE YAPOKEA RASIMU YA KATIBA MPYA



Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi iliyoketi Mjini Dodoma Chini ya Mwenyekiti wake DK JAKAYA KIKWETE imeipokea Rasimu ya Katiba mpya na kukiagiza chama kujipanga kuijadili rasimu hiyo ndani ya chama kama baraza la kitaasisi ili kupata maoni ya Wanachama juu ya mapendekezo yaliyotolewa.
Akitangaza maazimio ya Kamati Kuu, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC CCM, NAPE NNAUYE amesema, ushiriki wa Chama cha Mapinduzi kama mabaraza ya katiba yamelenga kuongeza idadi ya wanachama watakaotoa maoni juu ya upatokanaji wa katiba mpya.
Mbali na mpango huo tayari Rasimu ya kwanza iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeainisha uwepo wa Serikali tatu hali inayowapa wasiwasi Wananchi wengi juu ya muundo wake na hapa NNAUYE anatoa msimamo wa chama ikiwa Wanachama watakubali mfumo huo.

No comments:

Post a Comment