Tuesday, 25 June 2013

LAZIMA NIFE KABLA YA KUFIKISHA MIAKA 40"...AUNT EZEKIEL

WAKATI vifo vikizidi kuwatafuna wasanii, staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefunguka na  kudai kuwa hawezi kuishi miaka mingi  na  atakufa mapema kuliko  watu  wanavyodhani. Aunt Ezekiel alifunguka hayo juzikati alipokuwa  akipiga  stori  na  mwandishi wetu jijini Dar ambapo alibainisha kuwa akijitazama mustakabali wa maisha yake basi anaona kabisa kuwa hawezi kufikisha hata miaka 40  kabla  hajafa.
“Daah! Sijielewi kabisa yaani kwa jinsi ambavyo najiona, nikifikisha miaka 40 ni bahati aisee, dunia sasa imebadilika sana,” alisema Aunt.
MARADHI YA NGOZI YAMFANYA ATAKE KUJIUA MARA MBILI.

Bofya video iliyopachikwa hapo chini umsikilize Sylvester Karanja akielezea masaibu yake ya jinsi alivyozaliwa katika hali ya kawaida kama binadamu wengine wasio na ulemavu wa aina yoyote ile, hadi alipopatwa na kipele katika ujana wake, kipele ambacho kilibadili muonekano wake na kumsababishia sononi ambayo ilimsukuma kutaka kuutoa uhai wake.

Anasimulia kuwa alijaribu mara mbili kufanya hivyo lakini kila mara alipojaribu, alikwama.

Je! Maisha yake ya sasa yakoje? Msikilize akizungumza, kwani ni nani ajuaye, huenda ikawa ni msaada kwa mtu mwingine aliyekata tamaa?
- See more at: http://rommyzcity.blogspot.com/p/city-gossips.html#sthash.6OxGC4c4.dpuf

No comments:

Post a Comment