Msanii wa hip hop Tanzania Langa Kileo amefariki dunia katika hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam. Langa alipelekwa hospitali akiwa hajitambui. Anadaiwa kuwa alikumbwa na Malaria kali sana, Hali iliyopelekea kukimbizwa Hospitali ya Muhimbili jana. Uchunguzi wa chanzo cha kifo chake bado unaendelea.
Msanii Langa aliwahi kutamba na kikundi cha Wakilisha pamoja na witness na sara ni miongoni mwa wasanii wakongwe wa bongo flava nchini Tanzania.
Chanzo: General, via JamiiForums
No comments:
Post a Comment