Akizungumza na kipindi cha XXL mwanamuziki
i Ommy Dimpoz alizungumzia tukio la yeye kulushiwa makopo
stejini mjini Dodoma lakini zaidi alizungumzia kauli aliyoitowa wakati
wa tuzo za Kili.......
"imeenezwa chuki kwamba mimi nimemtukana
marehem Albert kitu ambacho sio kweli, nimejaribu
kukielezea kwenye media mbali mbali kuwa si kweli, wametumia kauli yangu
niliyoongea kupitia Killi siku ya Tanzania Music Awards wakati
kitu nilichokiongea nitofauti na kitu kilichokuja
kupandikizwa, lakini mi najua safari ya mziki ni ndefu, na
mwenyezi mungu atajaalia tu haya mambo
yatakwisha kwasababu hata yeye mwenyewe anajua
sina kosa, sija mkosea mtu wala sina tatizo na mtu, nafanya tu
maisha yangu ya mziki, lakini inapofikia time unajua mtu mwingine anaweza
akaja tu na sababu zake binafsi kwa nia ya kukuvuta
shati, lakini kama mungu amendika njia yako
nyeupe basi itakuwa nyeupe tu, na hakuna njia iliyonyooka siku zote lazima
inakua na vikwazo kidogo, kwa hiyo naamini hii ni
mitihani tu itaisha kwasababu sina tatizo na mtu.
nachoamini
binaadam tunakufa pengine roho pengine zinabaki zina hang, hata marehem
mwenyewe naimani anajua kwamba sikumtukana...................
hii ni challenge tu naichukulia kwangu,
pengine
ni mitihani kwasabau sijawahi kuipata na
ku experience katika maisha yangu ya mziki hiki ni kitu kikubwa
nimekutana nacho kwa sasa, lakini naimani itakwisha."
No comments:
Post a Comment