Umoja
wa mataifa unasema kuwa kiongozi mmoja mkuu wa kundi la wapiganaji wa
kiisilamu nchini Somalia, al-Shabab, Hassan Dahir Aweyes, amejisalimisha
kwa wanajeshi wa Somalia.
Bwana Aweyes alitafuta hifadhi mjini Adado,mji ulio umbali wa
kilomita miatano kaskazini mwa Mogadishu baada ya mapigano makali kati
ya mirengo ya Al Shabaab mwishoni mwa wiki.
Viongozi wa kiukoo, wamekwenda huko kujadili watakachofanya naye baada ya kujisalimisha kwake.
Lakini viongozi hao wamefahamisha mwandishi wa BBC kuwa amekanusha
madai kuwa amejisalimisha na kwamba amekataa kusafiri kwenda Mogadishu.
Bwana Aweyes amekuwa akijulikana kama kiongozi mkubwa katika kundi la
al-Shabab na Umoja wa mataifa na Marekani zinamfahamu kama gaidi
No comments:
Post a Comment