Wednesday, 26 June 2013

Kuhusu Afya ya Mzee Nelson Mandela Hiki ndio kinachoendelea huko Afrika Kusini

Kwa Mujibu wa BBC, Mandela anaendelea kupokea matibabu hospitalini, na Askofu mkuu wa kanisa la kianglikana mjini Cape Town, Afrika Kusini, Thabo Makgoba, amejitolea kufanya maombi kwa niaba ya rais mstaafu Nelson Mandela ambaye anaugua sana hospitalini.
Kasisi huyo anamuombea Mandela aweze kupata nafuu na amewataka wananchi kumshukuru kwa yote aliyowafanyia.
Maombi hayo yalitolewa baada ya Askofuu huyo kumtembelea Mandela hospitalini ambako kiongozi huiyo wa zamani amekuwa akilazwa kwa wiki mbili na nusu zilizopita baada ya kuugua mapafu.

Habari inayoleta wasiwasi mkubwa juu ya Mustakabali wa Afya ya Mandela ni hatua ya wajukuu wa rais huyo wa zamani wa Afrika kusini wanakutana nyumbani kwake kijijini katika mkoa wa Eastern Cape province, ambako viongozi wa kitamaduni wamealikwa kujadili mambo ambayo bado hayajafahamika kwa uhakika, wakati pia ndugu zake wengine wamekutana nyumbani kwake huko Kunu, huku hali yake ya afya ikizidi kudorora hospitalini, Pretoria.



Helikopta za jeshi pia zimeonekana zikipaa karibu nyumbani kwa Mandela na bado mpaka sasa hakuna taarifa zozote za kuimarika kwa Afya ya mpigania uhuru huyu.

No comments:

Post a Comment