Maombi yamefanyika leo katika makanisa mbalimbali nchini Afrika Kusini kumuombea hauweni mzee Mandela anaye endelea na matibabu Hospitalini mjini Pretoria.
Taarifa kutoka Ikulu zinaeleza kwamba Mandela ambaye ana umri wa miaka 94 anapumumua mwenyewe pasi na usaidizi wowote anaumwa mno lakini hali yake ina imarika alisema msemaji wa Mzee Mandela.
Rais Jacob Zuma ameashilia kwamba atamtembelea Mandela punde tu Madaktari watakapo toa Ruhusa.Hii ni mara ya tatu kwa Mzee Mandela Kulazwa Hospitali katika muda wa miezi sita iliyo pita.
Msemaji wa chama tawala cha ANC,Keith Khoza anasema anaimani kuwa mzee Mandela atapona.
No comments:
Post a Comment