Thursday, 27 June 2013

OMMY DIMPOZ APATA SHAVU LA KUFANYA TOUR MAREKANI NA CANADA


Omary Fereji Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz, amesaini mkataba na kampuni ya DMK Global Promotion leo hii kwa ajili ya tour atakayoifanya Canada na Marekani mwezi wa tisa mwaka huu baada ya kumaliza tour nyingine barani ulaya.

"Yaah nimesaini mkataba na nitaondoka kwenda kwenye tour hiyo mwanzoni mwa mwezi wa tisa, imekuwa hivyo kwasababu tunasubiri mwezi mtukufu upite si unajua tena, kampuni niliyosaini nayo inaitwa DMK global promotion ambayo ni ya mtanzania ambae anaishi marekani." amesema Dimpoz 

Alipoulizwa  kuhusu mkwanja alioingiza kwa mkataba huo, Dimpoz aligoma kutaja kiasi na kusema 

"aaaah unajua tena kwa matatizo yaliyotokea nikitaja tena na mkwanja nilioingiza si ndio itakuwa matatizo kabisa? .

No comments:

Post a Comment