M2 The P – Sijui ni nini kilichotutokea
Picha ya M2 the P na marehemu Ngwair, waliyopiga usiku wa dhahamaMsanii ‘M2 the P’ ambaye alikuwa na marehemu Albert “Ngwair” Mangweha nchini Afrika Kusini wakati rapper huyo anafariki na yeye kuzidiwa hadi kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi, afunguka kuhusu yaliyowakuta yeye na marehemu Ngwea
‘M2 the P’ ambaye awali naye aliripotiwa kuwa amefariki kabla ya taarifa hizo kukanushwa, alisema jana kuwa hadi sasa hajui nini kiliwatokea.
Msanii huyo alisema kwamba hakumbuki kilichotokea hadi wakazidiwa na kukimbizwa hospitali wakiwa hawajitambui. Alisema pia bado anajisikia anaumwa hadi sasa licha ya kuruhusiwa kutoka katika hospitali ya St. Hellen Joseph ya Afrika Kusini alikokuwa amelazwa. Source: IPP Media
No comments:
Post a Comment