Monday, 10 June 2013

MSANII WA BONGO MOVIE KASH AFARIKI DUNIA MUDA HUU

Habari iliyotufikia hivi punde ni kwamba msanii wa filamu nchini Jaji Khamis (Kashi)aliyewahi kutamba na michezo ya ITV enzi zile akiwa na wasanii kama mzee masinde,samson na wengine katika mchezo wa Tamu chungu na mingine mingi Amefariki dunia mchana huu katika hosptali ya taifa ya muhimbili alikokuwa amelazwa,akizungumza na the super stars tz raisi wa shirikisho la wasanii amesema kuwa tasnia yake bado inaendelea kukumbwa na majanga  lakini amedai yote ni kazi ya mungu
Nae mzee masinde ambaye alikuwa nae katika kundi moja akiwa kama kiongozi wake amesema kashi ni msanii ambaye alikuwa mpiganaji na kwa hakika ni pigo kubwa katika tasnia yetu
Mungu ailaze roho ya marehemu Jaji Khamis (Kashi)
mahali pema peponi Amini.

No comments:

Post a Comment