Hii ndio hali halisi kwa sasa huko Arusha
Baadhi ya watu waliopatwa na mahafa ya mlipuko huo wakiwa wanasaidiwa na wasamalia wema
Habari
zilizotufikia hivi punde kutoka chanzo chetu cha habari kutoka jijini
Arusha zinasema kwamba kitu kinachosadikika kuwa ni bomu limelipuka
kwenye mkutano wa chadema jijini Arusha limeua watu wawili na kujeruhi
wengine.
Na
gari la hospitali limevunjwa vunjwa vioo na watu wanaosadikika kuwa na
hasira kali baada ya kuchelewa kuwachukua majeruhi hospitalini wakati
hali zao ni mbaya. Na hivi sasa watu wanatumia magari yao binafsi
kuwapeleka majeruhi hospitalini . Napia kamanda mkuu wa mkuu wa mkoa wa
Arusha yuko kwenye eneo la tukio lakini bado hajangea na vyombo vya
habari.Mpaka sasa mlipuko huu chanzo chake hakijajulikana
No comments:
Post a Comment