Ni siku nne zimepita imetokea hali ya sintofahamu baada ya mpiganiaji Uhuru wa South Africa Babu Nelson Mandela kukimbizwa hospitalini baada ya hali yake kuwa mbaya na kuwekwa kwenye chumba cha watu mahututi..
... Ripoti kutoka kwenye hospital aliyolazwa Rais huyo wa zamani wa Taifa hilo inasema usiku wa kuamkia leo siku ya Alhamisi majira ya saa 8 usiku hali ya Mandela ilibadilika na Team ya madaktari walikusanyika na ilionekana Mapigo ya Moyo kuacha kufanya kazi kwa muda na Figo kushindwa kufanya kazi kwa dakika zisizopungua 10.... baada ya kupigania uhai wake hali ilirudi kuwa ya kawaida na kuendelea kupata matibabu chini ya madaktari Bingwa... Pia Raisi wa sasa wa South Africa Bwana Jacob Zuma ameongea na kusema ''Naiamini team ya madaktari inayomuangalia mzee wetu na nina imani Mungu atamuepusha na mabaya yote na kurudi kwenye hali yake kama kawaida...,nampenda mzee mandela, wote tunampenda mandela na dunia nzima inampenda kwahiyo kwa pamoja tuungane kumuombea...! |
No comments:
Post a Comment