Toka huu msiba umetokea kumekua na habari ambazo zinaandikwa au kuripotiwa lakini hazina usahihi, pia habari ya kusafirishwa kwa mwili imeandikwa tofautitofauti kwenye vyombo mbalimbali lakini uhakika ni kwamba mwili wa Marehemu umepelekwa Airport ya Johannesburg June 3 2013 ambapo utasafirishwa june 4 kuelekea Dar es salaam na kufika mchana saa nane.
Hizi picha zimepigwa makusudi ili kutoa ushahidi kwa wale ambao bado walikua hawaamini kama mwili huu umefikia kwenye hatua za kusafirishwa kutokana na kuahirishwa kusafirishwa mara mbili kwa sababu ya taratibu za Serikali ya Afrika Kusini ambazo ilikua ni lazima zifatwe hasa ikizingatiwa kwamba Marehemu ni kutoka nje ya nchi hii na kifo chake ni cha ghafla.
No comments:
Post a Comment