MWIGIZAJI wa kike na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Snura Mushi
amedai kuwa muziki ulimpa dili ya kwenda kurekodi filamu Afrika ya
Kusini, anasema kuwa watayarishaji wa filamu ya Tandeka iliyorekodi
jijini Pretoria kwa kuwashirikisha wasanii watanzania waishio Afrika ya
Kusini imetokana na kufanya vizuri katika muziki hasa nyimbo yake ya
Majanga.
.
“Filamu kwa sasa inachangamoto sana hilo lilinifanya nirudi katika
muziki huku nikichagua filamu za kuigiza na kujikita katika muziki zaidi
ambao unanifanya niwe bussy sana, lakini ninachofurahia kupitia nyimbo
yangu ya majanga nilipoenda kuirekodia Afrika kusini pia nilipewa
uhusika mkuu kuigiza filamu ya Tandeka,”anasema Snura.
Snura anadai kuwa watayarishaji walimuona na kumwita katika usahili
aliposhinda alipewa muswada (Script) na kuigiza kama mhusika mkuu ambaye
aliigiza kwa umahiri mkubwa filamu ya Tandeka imetumia lugha mbalimbali
ikiwa Kiswahili, Kizulu na Kiingereza, Snura ni msanii mwigizaji wa
filamu aliyetokea katika tamthilia ya Jumba la Dhahabu.
No comments:
Post a Comment