Kwa kile kinachoelezwa kupisha zoezi la upulizwaji wa madawa ya kuua wadudu na mazalia yake katika wodi za wagonjwa za Kibasila na Mwaisela, hospitali ya Mhimbili ililazimika kuwalaza nje wagonjwa ili kupisha zoezi hilo. Hali hii iliwashtua wengi kutokana na ukweli kwamba, kulaza wagonjwa nje ni hatari kwa afya zao! Lakini jambo hili linaweza kuonekna ni la kupuuzwa, huu ni ukweli kwamba bado sekta ya afya ina mahitaji makubwa sana ili kukidhi mahitaji ya Watanzania.
No comments:
Post a Comment