Tuesday, 23 July 2013

Kelly Rowland aokolewa baada ya kupotea baharini kwa masaa 12



Wasamwahi huwa tunasema "maneno huumba", nikiangalia hii story inayomuhusu Kelly Rowland kuokolewa baharini, nakubaliana kabisa pale nikiifikia video ya wimbo wa Destinys Child "Survivor" ambayo kuna kipande kinamuonyesha Kelly akiwa katikati ya bahari huku akiwa hajui pa kuelekea.
 In reality hii imetokea  kwa Kelly siku ya Ijumaa ambapo aliokolewa baada ya kukaa baharini na kutokujua wapi pa kuelekea kwa masaa 12.
Rowland na wengine nusu dazeni walikuwa kwenye chombo cha baharini kwaajili ya kwenda kujionea  nyangumi  (Ijumaa asubuhi) wakiangalia kujiingiza katika nyangumi, lakini ghafla walikutana na wimbi lenye urefu wa futi 5 na kusababisha ukungu, hatimae kuwapotezea muelekeo.
Nahodha wa meli akawa dhaifu na hajiwezi kutokana na hali hiyo, hata hivyo Master wa bandari alifanikiwa kupiga mahesabu yake na kufanikiwa kurudisha meli hiyo .
Nahodha Nuhu Santos alifawaokoa kila mmoja na kuwarudisha mida ya saa 5 ya Ijumaa usiku huku kila mmoja akiwa anatetemeka kivyaake.
Santos anasema siku ya pili yake, alipokea shukran binafsi kutoka kwa Rowland mwenyewe alipokutana nae  akiwa na mkewe out kwa ajili ya dinner, na Kelly aliwalipia chakula walichokula. Mpaka dakika hii Kelly hajaongea lolote juu ya hilo.
Kelly akiwa na aliemuokoa


No comments:

Post a Comment